September 14, 2021


 MFUNGAJI wa bao la kwanza la mashindano kwa msimu wa 2021/22 ndani ya kikosi cha Azam FC, Ayoub Lyanga yupo chini ya uangalizi mkali wa jopo la madaktari wa Azam FC ili kuweza kumpa huduma itakayomrejesha uwanjani.

Lyanga aliyepachika bao mbele ya Horseed FC katika mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho alikwama kuyeyusha dakika zote 90 Uwanja wa Azam Complex baada ya kupata maumivu ya mguu alitoka dakika ya 81.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit alisema kuwa nyota huyo atakuwa kwenye uangalizi kabla ya kurejea uwanjani kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa marudio.

“Lyanga hakupata majeraha makubwa ila baada ya mchezo ule kumalizika wachezaji walipewa muda wa mapumziko na wanatarajia kuanza mazoezi leo, (Jana) jioni kwa Lyanga kabla ya kuanza mazoezi atafanyiwa uchunguzi na madaktri ambao watatoa taarifa kwamba kama anaweza kuanza mazoezi au la,” alisema Thabit.

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati alisema kuwa wanahitaji kupata ushindi kwenye mchezo wao wa marudio ili waweze kutinga hatua ya makundi.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Septemba 18, Uwanja wa Azam Complex na Horseed FC wao walifunga bao moja huku Azam FC ikiwa na mtaji wa mabao matatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic