UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa umesajili wachezaji wa kazi jambo ambalo linawafanya wasiwe na hofu yoyote kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United.
Leo, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa awali dhidi ya Rivers United kutoka Nigeria ambao wa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mashabiki wasiwe na presha juu ya wachezaji wao watatu kukosa vibali vya kazi, (ITC).
“Ukizungumzia Yanga hauzungumzii mchezaji mmoja ama wawili ni orodha ya wachezaji wa kazi zaidi ya mmoja na tumesajili wachezaji 30 hii ina maana kwamba akikosekana mmoja mwingine anacheza.
“Kuhusu Aucho pamoja na maneno ambayo yanaendelea kwenye mitandao hayatupi hofu, tunahitaji kufanya vizuri na tutaonesha kazi uwanjani,” amesema Bumbuli.
Wachezaji ambao kunahatihati ya Yanga kuwakosa leo Uwanja wa Mkapa ni Khalid Aucho ambaye ni kiungo, Djuma Shaban ambaye ni beki pamoja na Fiston Mayele ambaye ni mshambuliaji.
Wanatamba wapi hao wanaweweseka tu kila kukicha
ReplyDeleteKila siku kufuatilia mambo ya Jangwani, ndiyo maana mlisahau kwamba Gomes alikuwa anatakiwa kwenda kwanza shuleni kujiongezea elimu ili aweze kukidhi video vya CAF.
DeleteVideo ya nini?Andika vizuri msukule. Wacha kuweweseka.
ReplyDeleteInauma Sana kuwa mwanachi
ReplyDeletena ubabaishaji unaendelea ndani ya Yanga.
Wanalalamika kupuungukiwa na wachezaji watatu tegemeo kwani lini au mara nagapi wachezaji hao walitumiwa katika mechi za maana hata kweli wakatambulikana kuwa kweli wachezaji hao tegemeo?
ReplyDelete