WAKATI tetesi zikieleza kuwa muda wowote Masau Bwire kuwa Ofisa Habari wa Ruvu Shooting atakabidhiwa mikoba ya Haji Manara, kiongozi huyo ameweka wazi kuwa kila kitu kitakuwa wazi hivi karibuni.
Ni Kaimu Ofisa Habari, Ezekiel Kwamwaga kwa sasa anashikilia kwa muda nafasi hiyo baada ya kupewa mikoba kwa muda wa miezi miwili na alibainisha kwamba ataondoka katika nafasi hiyo.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Bwire ambaye wengi hupenda kumuita mzee wa kupapasa alisema kuwa:”Hizo za kuhusu mimi kwenda Simba ni tetesi zipo kila kona, siku ikifika watu watajua pale wenye mamlaka watakaposema.
“Unajua mimi ni mzalendo si kwa Simba tu hata kwa Yanga nimefanya sana kutoa hamasa hasa kwenye masuala yanahohusu taifa.Mimi nina kawaida ya kuhamasisha pale timu inapokuwa na jambo linaloihusu Tanzania kwa kuwa ninajua hiyo ni fursa.
“Najua haya yametokana na watu kuona mimi nikizungumzia kushusiu Simba lakini hii Simba day kuna watu wanafuatilia nje ya Tanzania, wakiona kuna nyomi, watu wanaona kuna kitu kinaendelea, tushirikiane Watanzania tuache roho ya korosho.
“Kwa mfano tarehe 25/11-15/12 kutakuwa na mashindano ya soka la wenye ulemavu na Tanzania itakuwa mwenyeji, mpaka wakupe fursa hiyo ni watu wamekuamini na mimi nitakuwa msemaji rasmi kwenye mashindano hayo makubwa yatahusisha timu 16 nna wanatafuta timu 8 zitakazoshiriki mashindano Uturuki hivyo Watanzania tuungane,” alisema Bwire.
Hivi karibuni, Kamwaga aliliambia Championi Jumamosi kuwa mchakato wa kumsaka Ofisa Habari ukikamilika kila kitu kitawekwa wazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment