September 27, 2021


 NYOTA Willy Edgar Mwampamba mali ya Mbeya Kwanza leo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.


Ilikuwa ni dakika ya 49 nyota huyo alieza kufanya hivyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mabatini, Kibaha wakati timu ya Mtibwa Sugar ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Bao hilo lilidumu mpaka dakika 90 kwa kuwa Mtibwa Sugar walikwama kuweza kuweka mzani sawa na kuruhusu pointi tatu kusepa mazima na Wanambeya Kwanza.

Ni rekodi tamu kwa Mbeya Kwanza ya Mbeya ambayo imepanda daraja msimu huu kwa kuanza na kusepa na pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar.

Kocha Mkuu Joseph Omog leo alikuwa jukwaani akiwatazama vijana wake wakipoteza mchezo huo wa kwanza wa ligi na kipa wake Mshery kuwa wa kwanza kutunguliwa ndani ya msimu mpya.

1 COMMENTS:

  1. Acha wapigwe tu kama hawakujiandaa vyema kwa ajili ya msimu wa 2021 /22 ngoja yawakute, huenda wakasingizia uwanja wao kugungiwa dakika za mwisho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic