September 8, 2021

 


MZAWA Mbwana Samatta na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania,  muda mfupi baada ya kunaliza kazi ya kukiongoza kikosi cha Tanzania katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia alikwea pipa.


Samatta alikuwa ni nyota kwenye mchezo wa jana uliochezwa Uwanja wa Mkapa na ubao ukasoma Tanzania 3-2 Madagascar. 


Ni pasi ya mwisho ya ushindi alitoa kwa Feisal Salum ambaye hakuifanyia  makosa aliijaza kimiani kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango.


Anakwenda kwenye majukumu ya timu yake ya sasa ya Antwerp FC atakayokuwa huko kwa msimu huu  wa 2021/22.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Asante wachezaji kwa kupambana, benchi la ufundi kwa maelekezo mazuri, Watanzania kwa dua njema, kwa kheri ya kuonana Tanzania, ".

4 COMMENTS:

  1. Ahsante pia Mabwana ila tungependa kuona serikali inaigharamia zaidi timu ya Taifa Kama timu yake kwa hali na Mali.Timu ya Taifa ni timu ya serikali TFF ni wasimamizi tu,watu wanaweza kusema serikali inamkono wake kwenye maendeleo ya Taifa ila nisubutu kusema mkono huo bado ni dhaifu mno.Tusiende mbali tuwaangalie tu simba na sasa hata Azam wanavyopambana na maandalizi ya timu zao kuelekea mechi za kiushindani kambi nje,kambi ndani ya nchi,ahadi na mabonasi na matunzo bora kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi yalioshiba. Tulitarajia Taifa Stars kuwa Zaidi ya klabu yeyote nchini inapokuja kwenye suala la maandalizi na matunzo kwa wachezaji. Kwanza siku zenyewe wanazokaa wachezaji kwenye kambi ya Taifa Stars ni chache itashangaza hizo siku chache kukawa na maandalizi ya tia maji tia maji. Tumepata kocha mzuri apewe ushirikiano wa kibingwa zaidi sio majaribio. Wachezaji tunao wengi wa zuri kutokana na ukweli ni kwamba Wachezaji wetu wengi ni vijana na kocha tulienae ni mtaalam wa soka la vijana tupewe nini tena?

    ReplyDelete
  2. Hongera kwa Mbwana Samatta, amecheza vizuri sana, kimsingi ndio chachu ya ushindi dhidi ya Madagascar

    ReplyDelete
  3. kazi jana sama gool ameifanya amepambana ila não wachezaji wetu wabadilike makosa Yale Yale bado kidogo jamaa wale waonyeshe umwamba

    ReplyDelete
  4. Pole.kijana Ila usikose.kuwepo mechi ya marudiano na Kongo umetoa mchango wako Jana was kiufundi umeonyesha ukomavu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic