September 21, 2021


 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Namungo, Hemed Morocco amesema kuwa uwepo wa washambuliaji wapya ambao ni David Molinga na Obrey Chirwa ndani ya timu hiyo kutaifanya iwe tishio kwa msimu mpya wa 2021/22.

Chirwa na Molinga wote kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa wachezaji ndani ya kikosi cha Yanga na kila mmoja alitimiza majukumu yake ndani ya timu hiyo kwa mara ya kwanza ndani ya ardhi ya Tanzania.

Pia Chirwa arirejea kwa mara nyingine na alikuwa ndani ya Azam FC ila baada ya mkataba wake kuisha alipewa mkono wa kwa heri msimu wa 2020/21.

Morocco amesema kuwa kuongezeka kwa wachezaji hao wenye uzoefu kunampa matumaini makubwa ya kuona kwamba wanaweza kufanya vizuri kwenye mechi zao ambazo watacheza.

"Molinga na Chirwa ni wachezaji wenye uzoefu wa ligi ya Tanzania lakini pia ni wachezaji wazuri katika eneo la ushambuliaji hivyo uwepo wao utakuwa na faida kwetu.

"Hakuna ambaye hajui kuhusu ubora wao wawapo uwanjani kwa namna ambavyo wamekuwa wakipambana kutimiza majukumu yao kuingia kwao ndani ya Namungo kutaiboresha safu yetu ya ushambuliaji," amesema.

Kwa msimu wa 2021/22, Namungo itafungua pazia kwa kucheza na Geita Gold ambayo imepanda ligi msimu huu na mchezo utachezwa Uwanja wa Ilulu.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic