September 4, 2021

 

HASSAN Mwakinyo, bondia Mtanzania amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Afrika, ABU katika pambano la uzito wa Super welterweight baada ya ushindi kwa TKO katika raundi ya nne.


Ilikuwa ni dhidi ya bondia Julius Indongo kutoka Namiba kwenye mchezo uliopewa jina la Mabingwa wa Ulingo uliochezwa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Ubungo Plaza.


Ilikuwa ni katika pambano la raundi 12, Mwakinyo alishinda katika raundi ya nne na kumfanya aweze kutetea taji lake.


Baada  ya ushindi huo Mwakinyo amesema kuwa ushindi huo ni kudra za Mungu na anashukuru kwa kushinda.


Kwa upande wa Mnamibia amesema kuwa haelewi imekuajekuaje akashindwa katika pambano hilo kwa kuwa anaamini katika uwezo wake.

1 COMMENTS:

  1. Hongera sana Mwakinyo kwa kupeperusha vyema bendera ya Nchi yetu. Nimefurahia zaidi ushindi kwa TKO maana hapo umeondoa ile hofu kuwa pengine umebebwa na mwamuzi na majaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic