September 4, 2021


 BIASHARA United haitaweza tena kucheza mechi zao za Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza kama ilivyokuwa mipango yao baada ya CAF kuukataa uwanja huo na sasa wawakilishi hao watakipiga jijini Dar es Salaam.

 

Tayari timu hiyo ilishaweka kambi jijini Mwanza kwa wiki mbili, lakini wameambiwa mechi yao ya awali dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti itapigwa Benjamin Mkapa, kwa vile Kirumba imeshindwa kukidhi vigezo vilivyotakiwa.

 

Meneja na Mratibu wa Biashara United amesema wamelazimika kubadili kila kitu kwani walikuwa Kirumba kwa zaidi ya siku 10 na wachezaji walikuwa wamezoea mazingira hayo hivyo wapo kwenye hatua za mwisho za kuhamishia kambi Dar ili kuanza upya maandalizi.


Timu hiyo ni miongoni mwa zile nne kutoka Tanzania zitakazopeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa msimu wa 2021/22.


Ni Simba na Yanga kwenye hatua za Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam FC na Biashara United katika hatua ya Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic