CRISTIANO Ronaldo, nyota mpya ndani ya Manchester United baada ya kurejea hapo kwa mara nyingine ikiwa imepita miaka 12 amemshukuru Edinson Cavani kwa kukubali kumpa jezi yake pendwa namba 7,
Hivyo ni uhakika kwamba msimu huu Ronaldo atavaa jezi namba 7 na Cavani yeye atavaa jezi namba 21 ambayo ilikuwa inavaliwa na Daniel James ambaye msimu huu atakipiga ndani ya Leeds.
Awali ilikuwa ngumu kwa Ronaldo kupewa jezi namba 7 kutokana na sheria za Ligi Kuu England kusajili namba za wachezaji mapema ila kwa ruhusu maalumu Uongozi wa Ligi Kuu England ulikubali kuwapa ruhusu United kufanya jambo hilo la usajili wa jezi namba kwa Ronaldo ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Juventus.
Mkataba wake wa miaka miwili ndani ya Manchester United una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja ikiwa atafanya vizuri raia huyo wa Ureno ambaye wakati anasepa ndani ya kikosi hicho alikuwa anavaa jezi namba 7 ambayo ni pendwa kwake.
Baada ya Manchester United kupewa ruhusu ya kufanya mabadilisho ya jezi na uongozi wa Ligi Kuu England, Ronaldo amesema kuwa hakutarajia kupewa namba hiyo kwa wakati mwingine ila jambo hilo ni kubwa kwake na hana cha kusema zaidi ya kumwambia asante Edi, (Cavani).
Ronaldo amesema:"Sikuwa na uhakika kama inawezekana kuwa na jezi namba 7 wakati mwingine tena, hivyo ninaweza kusema kuwa shukrani nyingi kwa Edi, asante sana kwa jambo hili kubwa," .
0 COMMENTS:
Post a Comment