September 27, 2021

 


BAADA ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wameomba msamaha kwa kilichotokea Uwanja wa Mkapa.


Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes haikuwa na bahati mbele ya Yanga baada ya kuokota bao dakika ya 10 nyavuni likadumu mpaka dakika ya 90.

Shomari Kapombe,  nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa hawakupanga kupata matokeo hayo ila imetokea bahati mbaya jambo ambalo wanaomba msamaha.

"Mchezo wetu uliopita hatukupanga kupoteza ila imetokea hivyo hakuna namna, kila mchezaji ameumia na tunatambua kwamba mashabiki wameumia kwa kilichotokea tunaomba msamaha.

"Kwa mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi kwani kazi bado inaendelea na kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Biashara United tuna amini kwamba tutapata matokeo," amesema.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa matokeo ya mchezo uliopita hawakuyatarajia hivyo wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Simba itamenyana na Biashara United kesho kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni msimu wa 2021/22.

4 COMMENTS:

  1. MZIDISHE JUHUDI YA KUPAMBANA BIASHARA WAZURI KULIKO YANGA...
    USISHANGAE KUSEMA HIVYO BIASHARA HAJATOLEWA KIMATAIFA ATI..

    ReplyDelete
  2. Juhudi? Baada ya kuzeekea kambini lakini kitu kizito kimewagonga.

    ReplyDelete
  3. Ila wewe ukuzekea kambini ulizekea ligi ya mabingwa ausio kawaida yenye mkimfunga simba mnaona mmemaliza kira kitu tukumbushane mwisho wa msimu

    ReplyDelete
  4. Yanga hana tofauti na mwanariadha wa mbo fupi,msiilaumu hata kidogo ilipaswa iwe hivi kwa lengo la kuwapoza washabiki wake kwa vipigo vitatu mfululizo walivyopata.mungu atadhihirisha mbona bado mapema sana,wataanza kusema refa wa simba kwani hata mechi ya juzi dabi walishaanza kusema eti refa ni mali ya simba.tumeshawazoea hawa,jana wenzao wametolewa jasho na wazee wa mji mkongwe costal na ukumbuke azam wanaonekana kua na kikosi bora zaidi ila angalia kilichowapata jana,ligi sio mechi moja ngoja tusubiri tuone.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic