September 1, 2021

 


SASA ni rasmi kuwa uzinduzi wa jezi za Klabu ya Simba itakuwa ni Septemba 4, saa 1:00 usiku.


Kupitia kwa Fred Ngajiro Mtendaji Mkuu wa Vunja Bei ambaye alishinda tenda ya jezi amesema kuwa jezi hiyo mpya ya Simba itakuwa ni nzuri sana na ya kipekee.


"Uzinduzi wetu wa jezi tutaizundua Septemba 4, saa 1:00 usiku na jezi yetu itakuwa nzuri sana kushinda jezi za timu nyingine hizi za ndani.


"Baada ya uzinduzi zitakuwa madukani na zitauzwa masaa 24, na nina amini kwamba ni bora," amesema.


Asubuhi ya leo Simba walitoa taarifa kwamba watakuwa na mkutano ambao utazungumzia masuala ya jezi.


Watani zao wa jadi Yanga tayari wameshazindua uzi mpya ambapo wanazo aina 10, kuanzia zile za viongozi, mashabiki, kitaifa na kimataifa.

Jezi inayotajwa kupendwa kwa Yanga ni ile ya njano yenye muonekano kama watu kwenye uzi huo wakiwa wanamaanisha kwamba wana watu.

Timu nyingine ambayo imezindua uzi mpya ni pamoja na Azam FC ambayo nayo inashiriki mashindano ya kimataifa kwa sasa ipo Zambia.

2 COMMENTS:

  1. Hehehe... za mwanzo zimefichwa

    ReplyDelete
  2. Hizi jazi za simba zinakwenda kuzinyea zile za Yanga. Nimependa jinsi Simba walivyo mafundi katika kuandaa Mazingira mazuri ya ununuzi wa jezi zao. Maana ya Yanga kama iliwashtukiza hivi mashabiki wao kwenye jazi zao. Naamini sio kila surprise ni jambo la kuhamasisha. Naamini simba day by far itakuwa Tamu kuliko ya Yanga. Simba Wana uzoefu na haya Mambo. Hayo matamasha ya ligi ya mabingwa peke yake ni uzoefu tosha ya vipi wanaweza kuujaza uwanja wa mkapa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic