WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen wana kibarua cha kufanya kwa ajili ya kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia kwa kucheza mechi mbili ndani ya mwezi Septemba.
Kila timu ambayo inakwenda uwanjani inahitaji ushindi hilo ni jambo la kwanza ambalo wachezaji wa Stars wanapaswa kulitambua.
Huu ni muda wa wachezaji Stars kuwapa furaha Watanzania kwa kuwa wanapenda kuona mnafanikiwa na kila kitu kiwe katika mstari.
Ujumbe wangu kwa wachezaji ambao wameitwa timu ya taifa ni lazima watambue kwamba wamekwenda kufanya kazi. Hilo lipo wazi wanapaswa wapambane mwanzo mwisho kuweza kuwa sawa katika mechi zao ambazo wanakwenda kucheza.
Juhudi kubwa ikifanyika uwanjani itaongeza uwezekano mkubwa wa kupata ushindi katika mechi ambazo mtacheza. Hivyo basi kila kitu kinawezekana na mkiwa ndani ya uwanja fanyeni kweli.
Ikiwa wachezaji mtashindwa kujituma kwenye kusaka ushindi itakuwa ni rahisi kwenye kukwama kufikia malengo yenu. Na kushindwa kufikia malengo ya kupata ushindi ni pigo kwa taifa.
Mkiwa kwenye jambo la kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa hapo kazi ni moja kupeperusha bendera ya Tanzania bila kuogopa ndani ya uwanja.
Ukweli upo wazi kwamba kila mchezaji ambaye ameitwa kuitumikia timu ya taifa uwezo wake upo wazi na hali hiyo imepeleka kila mmoja akapata nafasi ya kuitwa kikosini kupambana na timu kwa ajili ya majukumu ya Tanzania.
Jambo la kuzingatia ni nidhamu na kuwa wasikivu kwa kile ambacho mwalimu anawaambia. Ikiwa mtafuata maelekezo ya benchi la ufundi itaongeza nguvu na ari kwa mashabiki kuendelea kuwafuatilia kwenye mechi zenu zote.
Taifa letu linapenda kufuatilia michezo na tunaamini kwamba mtakwenda kufanya vizuri huko ambako mtakuwa mnacheza.
Muhimu kufanya kazi kwa nguvu bila kuchoka hiyo itasaidia matokeo kupatikana kwa sababu hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.
Makosa ambayo mtakuwa mnayafanya ni lazima mrekebishane wenyewe kwa wenyewe na kuamua kuzungumza lugha moja ya kusaka ushindi.
Hii itazidi kuwafanya mzidi kuwa sokoni kwa kuwa kadri mnavyofanya vizuri mnazidi kuwa kwenye ramani ya kuwa sokoni hasa kwa wale ambao wanawafuatilia.
Wachezaji pambaneni bila kuchoka ndani ya uwanja ili kuweza kufanya vizuri. Ushindani upo wazi ndani ya uwanja nanyi pia ongezeni juhudi katika kusaka matokeo.
Jambo kubwa la kufanya ni kukubali kujifunza na pale ambapo mnakosea ndani ya uwanja mna kazi ya kurkebishana wenyewe kwa wenyewe ili kusaka matokeo kwenye mechi zenu ambazo mtacheza.
Kila mchezaji anapenda kuona timu inapata matokeo mazuri. Ikiwa morali itakuwa kubwa kwa kila mchezaji itaongeza nguvu pia ya kupata matokeo mazuri wakati ujao kwenye mechi za ushindani.
Hakuna ambaye atapenda kushindwa kupata matokeo kwa namna ambavyo wachezaji wamekuwa wakifanya maandalizi basi yote yazingatiwe na yafanyiwe kazi.
Mbele ya DR Congo pamoja na Madagascar ni lazima kila mchezaji ajitoe na kushirikiana na wachezaji wengine. Ushirikiano ni jambo la lazima ili kuweza kushinda na kila mchezaji ana deni la kulipa kwa mashabiki wa Tanzania.
Na timu hii?
ReplyDelete