UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa walifanyiwa mbinu mbaya ili kuwatoa mchezoni na wapinzani wa Rivers United katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika nchini Nigeria.
Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Mawasiliano ndani ya Yanga, Hassan Bumbuli ameweka wazi kuwa walifanyiwa mambo ambayo sio ya kiuungwana ikiwa ni mbinu ya wapinzani wao.
"Tunamshukuru Mungu tumemaliza mchezo wetu salama na tulipata nafasi kama tatu hivi ambazo zilikuwa ni penalti za wazi ila mwamuzi akapeta nazo.
"Wenzetu walikuja na ajenda ambapo wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza walikuwa wanatajwa kuwa wana COVID 19 lakini wameshindwa kuthibitisha hilo.
"Tunashukuru kwa ajili ya wachezaji wetu ambao waliweza kupambana kwa ajili ya timu na mwisho wa siku tumeshindwa kupata kile ambacho tulikuwa tunatarajia.
"Tumepata somo kubwa katika hili hasa kwenye upande wa COVID 19. Tunarudi kujipanga kwa ajili ya mashindano mengine, mashabiki wasiwe wanyonge bado tupo imara na tuna kikosi kizuri," amesema Bumbuli.
Wachezaji ambao walikuwa wanatajwa kuwa na COVID 19 ni Yacouba Songne, Mukoko Tonombe, Feisal Salum pamoja na kipa Diarra ila mwisho wa siku wote waliweza kucheza mchezo huo jana.
Nchini Nigeria Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kufanya itolewe kwenye Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 2-0 kwa sababu kwenye mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Tayari kikosi cha Yanga kimerejea Dar leo Septemba 20 kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 kazi yao inayofuata ni Septemba 25 itakuwa dhidi ya Simba, mchezo wa Ngao ya Jamii.
Wao wamesahau waliwapachika wenzao corona na kuwapiga nondo jui. Ubaya haujengi yanga wajifunze uingwana na wacheze mpira sio malalamiko kila kona.
ReplyDeleteWanawapachika vipi? Basi ni kweli mlivywapachika wachezaji 5 wa Platinum
DeleteKwa kweli Yanga mmetuabisha sana sisi wapenzi na mashabiki wa timu. Kila mara ni kujitungia sababu zisizo na mashiko.
ReplyDeleteHivi ni hujuma gani wanayo lalamikia kufanyiwa ilihali wachezaji wote walicheza!!? Au ndio wanatafuta visingizio! Poleni Utopolo ila kwa kweli mmetuangusha sana sisi tuliojitahidi kukubebeni
ReplyDeleteMimi mwenyewe sijawaelewa kabisa, Kupigwa wamepigwa Tu na wametolewa. Na Bahati Yao wanatafuta Faraja kwa Mgongo wa Simba Day.
Deletemsituombee mabaya na mzee mpili wenu 😄😄😄😄 ili tuje tuwabebe tena 😂😂😂😂
ReplyDeleteTujifunze kukalimu wageni, lakini pia Tujifunze kuwa wamoja.Simba wameonesha ukimya hawakuweza kushadadia Ujio wa Rivers kama Yanga walivyokuwa wakifanya kipindi cha Wageni wa Simba SC 🦁 Msimu uliopita
ReplyDeleteYanga wanahitaji bado kuendelea na mazoezi yao kwani hata kocha alusena muda haukutosha. Makoro kocha alishasema wamekamilika kwani muda uliruhusu lakini wakapigwa
ReplyDeleteKwani ukikamilisha programu maana yake haufungwi? Si inategemeana na mpinzani wako? Mmmoja amefungwa na Riveriars ya Nigeria, mwingine amefungwa na TP Mazembe ya Afrika, hapo utapima mwenyewe
DeleteShida ya yanga walijiamini mno, walitegemea zaidi sifa wanazomiminiwa na magazeti ya udaku, mazoezi na mbinu zimeishia kwenye magazeti, wenyewe wanavyosifiwa na magazeti basi ndio wanafikiri wameshamaliza kazi kweli. Yanga kuweni na mipango endelevu na kuweka sifa za magazetini pembeni.
ReplyDeleteMnabahati mpira haukuonyeshwa, vinginevyo mngeumbuka na penalty zenu za uongo. @msukule aliwahi kuwaita Malalamiko FC. Amethibitisha kuwa ni kweli. Au TFF ya Karia inawahujumu.
ReplyDeleteWalah,, hakuna game wanafungwa hawa watu bila kukutajia penati walizonyimwa!
DeleteKumbe yanga mlikuwa tena full squad?? Na tena yule kipa mdaka mishale kashindwa kudaka mpira tena hd mkafungwa???? Me nlidhan yanga iliondolewa mchezoni kwa kuwakosa nyota wake muhimu, kumbe cyo??? Doh! Poor yanga
ReplyDelete