September 27, 2021

 


KAIMU Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amesema kuwa kushinda kwao Ngao ya Jamii ni mwanzo mzuri wa kwenda kutwaa makombe yote ya msimu huu.

 

Senzo alifunguka kuwa hakuna jambo nzuri kwa timu yoyote ile duniani kama kuanza msimu kwa ushindi au ubingwa na jambo nzuri kwao wameanza kwa kuifunga Simba ambao ni watani wao.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Senzo alisema kuwafunga Simba na kuchukua ubingwa ni kitu kikubwa kwao tofauti na watu wanavyofikiria kwa sababu hiyo itawaongezea morali na ari kuelekea kuanza msimu mpya wa ligi.

 

“Nafikiri hii sasa ni ishara ya kuwa makombe yote ya msimu huu ni ya kwetu, kumfunga Simba na kuchukua kombe ni jambo ambalo linatengeneza kitu cha utofauti kwenye timu.

 

“Watu wanajua kuwa hatuna mafanikio kwa misimu minne sasa, hivyo huu unakwenda kuwa msimu wa mataji kwa Yanga,” alisema Senzo.

 

Yanga waliwafunga Simba bao 1-0 na kutwaa Ngao ya Jamii kwenye mchezo ambao ulichezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa.

6 COMMENTS:

  1. Ivi viongozi wa yanga wanakuwaga na akili nzuri? Ligi mnacheza Pekee yenu mshinde sote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hayo ni malengo au nyie mnajipangia mechi za kufungwa?

      Delete
  2. Mlivyofungwa kigoma mbona hukusema kitu?

    ReplyDelete
  3. Timu iko vizuri zaidi na hapo bado muunganiko! Dua lenu halitabadilisha kitu

    ReplyDelete
  4. Muunganiko unaujua wew apo ndyo tayali itakuwa ivyo ivyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic