October 13, 2021

 


UONGOZI wa Biashara United umeweka wazi kuwa kwa sasa vichwa vinawauma kuhusu suala la usafiri wa wachezaji wao kuelekea nchini Libya kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Tripoli.

Biashara United ina kibarua cha kusaka ushindi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya kwanza dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya ambao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 15, Uwanja wa Mkapa.

Seleman Mataso, Mwenyekiti wa Biashara United amesema kuwa kuhusu mchezo wao wa nyumbani hawana tatizo ila kinachowaumiza ni ule wa marudio nchini Libya hali ni mbaya.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mataso alibainisha kuwa wanahitaji kufanya vizuri kimataifa ila hali ni tete kwenye upande wa mkwanja.

“Hali ni mbaya sana kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio ugenini, kwa muda huu gharama za matumizi ya safari mambo hayajakaa sawa na hata tiketi pia bado hatujapata hivyo wadau watupe sapoti katika hili,” .

Biashara United inayonolewa na Kocha Mkuu Patrick Odhhiambo iliweza kufika katika hatua hiyo baada ya ushindi mbele ya Dikhil.Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Oktoba 23 nchini Libya.

 Imeandikwa na Dizo_Click

10 COMMENTS:

  1. Ndio wakome, wako wapi waliokuwa wanajiita walezi na kumwanga mpunga kuiharibia simba?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa hiyo wangewaachia Simba washinde ndio wangewalipia ticket !!!

      Delete
    2. Hela waliowaandalia kuifunga Simba ingekuwa na tija zaidi kama ingetolewa mchango kuwezesha timu kusafiri.

      Delete
  2. Wale walioahidi kuwapatia hela endapo wangeifunga Simba wajitokeze sasa

    ReplyDelete
  3. Muda huu hutawaona hao wafadhili fake, subiri wakicheza na simba. Hiyo ndio faida ya kutumiwa kama toilet paper.

    ReplyDelete
  4. Mimi mtizamo wangu mkoa wa Mara, TFF na wadau wengine wapenda michezo ni wakati sahihi wakizipiga tafu timu zinakuwa zinawakilisha Nchi ukiziondoa Simba, Yanga na Azam.
    Kwa sabbu uwekezaji mkubwa umejikita kwenye Vilabu vitatu tu, tusinyoosheane vidole kutafuta nani alaumiwe kwa hili la biashara.

    ReplyDelete
  5. Hili la Biashara liwe fundisho kwa mikoa iliyo na timu kwenye ligi zetu.
    Kushindwa kwenda kucheze mchezo wa marudiano naamini tunaijua adhabu yake, kumbukeni mtibwa ilipigwa adhabu gani.
    Chonde chonde wadau tuisaidie timu ipate kusafri.

    ReplyDelete
  6. 2004 mechi ya mtibwa na Santos ya Afrika kusini ilishindikana kuchezwa marudiano Africa kusini mtibwa walikosa hela za usafiri.
    Walipigwa adhabu.

    ReplyDelete
  7. Wakati umefika kuongeza motisha kwa wachezaji kama ni zao au walitoa kwa jamaa..... mungu siyo Athumani....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic