October 12, 2021



KITENDO cha mabosi wa Yanga kushindwa kujibu tuhuma za kuwafanyia vurugu wapinzani wao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Rivers United inaelezwa kuwa kimewagahrimu faini ya milioni 11.

Imeelezwa kuwa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) limeipiga faini hiyo Yanga kwa kushinda kujibu tuhuma za kuwafanyia fujo baadhi ya watu waliokuwa kwenye msafara wa Rivers United ya Nigeria.


Malalamiko hayo yametokana na mechi ya hatua ya awali iliyochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United.

Rivers waliweza kuripoti Caf na kupitia mitandao ya kijamii ya timu hiyo walilalamika kupigwa kwa watu wao ikiwa ni pamoja na Ofisa Habari wa timu hiyo, Charles Mayuku.

CAF imesema mechi hiyo haikutakiwa kuwepo mashabiki ila walibaini baadhi ya mashabiki uwanjani jambo ambalo limesababisha pia Yanga kupigwa faini.

Habari kutoka Yanga imeeleza kuwa kwa sasa ishu hiyo bado haijawa rasmi zaidi ya kuwa tetesi.

4 COMMENTS:

  1. Safi kabisa! washenzi ni vizuri tu wasicheze kimataifa. Walizoea kuwafanyia fujo mashabiki wa Simba...kuwapiga kuwachania nguo zao.Hatushangai wakifanya kama kile walichomfanyia Kibu Denis

    ReplyDelete
  2. Wao wanajiona miamba na hawaogopi chochote wala yeyote

    ReplyDelete
  3. Tatizo yanga wamezoea kudekezwa na TFF kwenye muendelezo wa kufanya bmambo ya hovyo wanayoyafanya kwenye ligi kuu. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo sasa matokeo yake ndio hayo Tena ila unakaa na kujiuliza SENZO ni CEO au mnyoo unaowatafuna Yanga? Mbona analala Sana na kushindwa kufanya majukumu yake ya kazi yaani hafikii hata robo ya ya utendaji kazi wa Barbara wa simba.

    ReplyDelete
  4. Bora wangepigwa adhabu kubwa zaidi wajifunze kuwa uhuni na vurugu sio sehemu ya michezo. Hii klabu ovyo sana na inatia aibu kubwa mno

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic