October 13, 2021

 


SHIRIKISHO la Soka Afrika, (Caf) limeipiga rungu ya faini ya milioni 11 Yanga kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kufanya fujo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United pamoja na kuingiza mashabiki kwenye mchezo huo.

Ikumbukwe kwamba Septemba 12, Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 kwenye mchezo wa awali ubao ulisoma Yanga 0-1  Rivers United, ilielezwa kuwa wapinzani hao wa Yanga walipeleka malalamiko Caf kuwa walifanyiwa vurugu pamoja na uwepo wa mashabiki kwenye mchezo ambao haukupaswa kuwa na mashabiki.

Taarifa kutoka Caf imeeleza kuwa Yanga walishindwa kujibu taarifa za tuhuma hizo za kuwafanyia fujo watu waliokuwa kwenye msafara wa Rivers United ya Nigeria pamoja na kubaini uwepo wa mashabiki uwanjani.

Akizungumza na Championi Jumatano,Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli aliweka wazi kuwa walipata barua hiyo ila wameshangazwa na hukumu hiyo jambo ambalo limewafanya wakate rufaa.

“Tulipokea barua Oktoba 5 na tulipaswa kuijibu, kabla hatujaijibu adhabu imetolewa, sababu ambazo zimetajwa tunaona kwamba ni suala la mashabiki hilo lipo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) sisi Yanga hatuhusiki na kwa upande wa vurugu ilikuwa ni stewart ambao wanasimamia hivyo tumewaandikia barua Caf kukata rufaa juu ya suala hilo,” alisema Bumbuli.


10 COMMENTS:

  1. Mimi nadhani TFF na hiyo CAF wanaendesha issue zao kiswahiba ,tumeona na tunaona the way vyama Kama UEFA wanavyofanya issue Kama hizi siyo short notice na wameisha kaa na kuhadhibu ,hii imetungwa na Kuna Walakini kwa Football adminstration tupo biased Lakini Yana mwisho na hii haitujengi

    ReplyDelete
  2. Wazee wa makesi kesi kila msimu ..... Mtumieni yule afisa malalamiko wenu a.k.a afisa mipasho, mliyemsajili kwa mbwembwe

    ReplyDelete
  3. Hapo TFF inahusikaje, yanga waache kujifanya wanajua sana sheria, kisa lilifanyika wazi wazi wajinga wenu walimpiga nondo mnaija sasa mnalalamika nini, lipeni wapuuzi sana nyie.

    ReplyDelete
  4. Kosa lilifanyika wazi wazi na mkashindwa kukitetea sasa rufaa ya nini

    ReplyDelete
  5. Watasema simba inahusika. Hao ndio uto bhana!!!!!

    ReplyDelete
  6. kosa limefanywa na yanga asa Tff wanausikaje apo akuna kukwepa lipeni tu hzo pesa ili mjifunze.

    ReplyDelete
  7. Kosa ni kosa lipa deni
    Ukweli mlifanya vurugu lipeni deni, hamna nidhamu kabisa nyie uto

    ReplyDelete
  8. Duuu kweli kuna watu mizigo hata mambo ya wazi...faini inapelekwa yanga au tff? Yanga waliingiza mashabik? Yanga Ndo wasimamiz wa uwanja?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic