October 7, 2021

 


KAMPUNI ya mchezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania imetumia jumla ya Sh. milioni 961 kuwazawadia washindi mbalimbali wanaobashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 na Jackpot Bonus .

Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi wakati wa kumzawadia zawadi yake Stephano Ndundulu kutoka mkoani Njombe aliyeshinda Sh104.3 millioni.

Mushi alisema kuwa Ndundulu anakuwa mshindi wa 10 kuzawadiwa mamilioni ya fedha kwa mwaka huu na kuifanya kampuni yao kutumia kiasi hicho cha fedha.

 Alisema kuwa wanajisikia faraja sana kuendelea kubadili na kuwawezesha wanamichezo kupitia michezo yao ya kubashiri na sasa kuwa na maisha bora.

“Mbali ya kubadili maisha ya washindi wetu kupitia kubashiri michezo, pia tunajisikia fahari kuchangia  asilimia 20 ya kodi ya ushindi ambayo inaigia moja kwa moja Serikalini . Sisi ni walipa kodi wazuri wa Serikali na tunachangia maendeleo,” amesema Mushi.

Ameongeza kuwa kati ya fedha hizo, Sh791millioni ni zawadi za moja kwa moja kwa washindi wakati Sh200 millioni ni zawadi kwa ya ‘jackpot’ bonus. 


Ameongeza kuwa wanatarajia kuwazadia washindi wengi  mwaka huu kwani ligi mbalimbali zinaendelea mpaka sasa.

Kwa upande wake, Ndundulu ambaye ni shabiki wa Yanga amesema kuwa hakuamini kushinda kiasi hicho cha fedha kwa kutumia Sh1,000 tu. “Mimi mkulima wa maharage, nimekuwa nikibashiri na kupata hela ndogo ndogo. Nilipopigiwa simu na kuambiwa kuwa nimeshinda zaidi ya milioni 100, sikuamini  na nilidhani ni ndoto,” amesema Ndundulu.

Amesema kuwa fedha hizo atazitumia kuendesha kilimo cha kisasa zaidi na kutoa ajira kwa watu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic