October 2, 2021

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuna wachezaji ambao wataukosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold kutokana na sababu mbalimbali.

Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa na ushindani lakini wapo tayari licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji.

Ni Bakari Mwamnyeto ambaye ni beki huyu alikuwa anatibu majeraha yake ila ameshapona na yupo tayari kwa mchezo ila atapumzishwa.

Pia Tonombe Mukoko ambaye ni kiungo huyu alikosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba pia aliwakosa Kagera Sugar na leo anakamilisha mchezo wake wa tatu kwa kuwa alikuwa na adhabu ya kadi nyekundu alionyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Simba katika Kombe la Shirikisho.

Pia wapo wale ambao wapo kwenye program maalumu ambao ni Mapinduzi Balama, Yassin Mustapha pamoja na Dickson Ambundo ambao hawa hali zao zinaendelea vizuri.

Bumbuli amesema:"Licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji kikosi kipo tayari kwa mfano Mwamnyeto huyu amepona lakini mwalimu anahitaji kuona anapata muda wa kuwa fiti zaidi,".

5 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Yanga ni timu peke yake iliotoka ikacheza ugenini na ikarudi kwa mkapa nakua mwenyeji timu zingine zimecheza mara mbili ugenini nadhani mmenielewa kinachoendelea

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic