October 6, 2021


AMISS Tambwe, mshambuliaji wa timu ya DTB inayoshiriki Championship amesema kuwa ligi hiyo ni ngumu kwa kuwa kila timu inapambana kufanya vizuri.

Mchezo wake wa kwanza nyota huyo raia wa Burundi aliweza kufunga mabao maane na kuweka rekodi ya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga hat trick ilikuwa mbele ya African Lyon. 

Katika mchezo mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru dakika 90 zilikamilika na ubao ulisoma DTB 4-1 African Lyon.


Tambwe aliyafunga mabao hayo dakika ya 12, 40, 46 na 54, huku lile la African Lyon likifungwa dakika ya 80 kupitia kwa Wilbart Mkimbu.


Mchezaji huyo ambaye amewahi kucheza Simba na Yanga kwa nyakati tofauti amesema:"Ligi Daraja la Kwanza ni ngumu kwa kuwa kila timu inapambana ili kufika juu.


"Haina tatizo kwa namna ambavyo tumejipanga tuna amini kwamba tutafanya vizuri na kila mchezaji anajua kazi yake ni katika kutimiza majukumu," amesema.

7 COMMENTS:

  1. Ligi ngumu halafu mtu mmoja afunge mabao 4 katika mechi moja??! Aache utani bwana!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hasani unajua kucheza mpira AU unaongea tu ???
      Hata timu ya mtaa wako unaweza kupangwa ???

      Delete
  2. Tambwe alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kufunga alipokuwa Sumba na Yanga ..sidhani km uwezowake ume umepungua sana..

    ReplyDelete
  3. Hamisi Tambwe Apewe Hongera SANA. Hata YANGA ya sasa aweza Kufanya VIZURI SANA kuliko Yakubu Sonye !
    Big up TAMBWE!

    ReplyDelete
  4. Kwanini YANGA isimsajili Makambo mwakani??? Maana yuko VIZURI Na munkari kuliko MAKAMBO NA KASEKE .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kumradhi, nasema kwanini YANGA isimsajili Hamisi Tambwe ???Apewe nafasi Ni mzuri kuliko MAKAMBO NA KASEKE kwa REKODI Na munkari .

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic