October 5, 2021


 NYOTA wa Yanga Jesus Moloko kwa sasa yupo zake DR Congo pamoja na beki Djuma Shaban ambao wote wameanza kuonyesha makeke yao ndani ya Ligi Kuu Bara.

Pia waliweza kucheza mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara  ule wa Ngao ya Jamii, Septemba 25, Uwanja wa Mkapa na ubao huo ulisoma Simba 0-1 Yanga na bao lilipachikwa na Fiston Mayele.

Wachezaji hao wawili wamerejea kwao kupata pasi mpya za kusafiria baada ya zile za awali kujaa kwa mujibu wa ripoti kutoka ndani ya Yanga.

Taarifa imeeleza kuwa wakikamilisha suala hilo watarejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara na mchezo wao ujao utakuwa dhidi ya KMC ya Dar.

"Wachezaji wetu wanafuatilia pasi ili waweze kuendelea kuwa ndani ya Yanga na wakimaliza watarejea kuendelea kutimiza majukumu yao.Kuhusu sehemu ambayo kambi itawekwa hilo lipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi," ilieleza taarifa hiyo.

Awali Nabi alieleza kuwa kikosi hicho kina mpango wa kuweka kambi Arusha kwa muda huu ambapo ligi imesimama.

Mchezo wao wa ligi wa Yanga utachezwa Songea Oktoba 19.

6 COMMENTS:

  1. Nilijua labd kweny timu ya taifa kumbe utumbo mtupu ilimradi isomwe...kichwa cha kipo kibiashar zaidi kuliko uhalisia wa taarifa lenyewe

    ReplyDelete
  2. Taifa kaitwa Enock verani wa mnyama wengine hao mhh☹️

    ReplyDelete
  3. Aende,na uwezo wake mdogo sana huwezi mlinganisha na bangala hata chembe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wenye uwezo mkubwa mbona hawaitwi au kwa sababu wapo timu ndogo?

      Delete
    2. machozi ya mtu amayelia akiwa amepanda Mercedes benz na aliyepanda baiskel yanatofautiana sana, kwanza aliyepanda baiskel akiambiwa shuka upande benz atafuta machozi na kuanza kufurahi, sawa sawa na bangala anavotamani kucheza msimbazi ndo maana anawaonea gele wenzie mpaka anajisahau anatukana

      Delete
  4. Acheni uzobo makolo nyie. Hakuna mchezaji wa Simba aliyeitwa National team ya Dr Congo. Simba wengi mazoba wanatafuta kiki kivungu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic