October 3, 2021

 


KIBU Dennis ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba sasa yupo huru kuitumikia Simba baada ya suala lake la vibali kukamilika na sasa rasmi ni raia wa Tanzania.

Kukamilisha kwa suala hilo sasa inakuwa rasmi Simba imepata jembe lingine la kazi kwa upande wa ushambuliaji ambao unaongozwa na nahodha mzawa, John Bocco, Meddie Kagere na Chris Mugalu hivyo anakuwa mshambuliaji wa nne.

Nyota huyo alikuwa hajaonekana katika mechi za awali za Simba kutokana na tatizo la uraia wake jambo ambalo lilipelekea pia jina lake kutokuwa katika orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars.


Taarifa ambayo imetolewa na Simba imeeleza kuwa yupo tayari kuitumikia Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ambaye anatajwa kukubali uwezo wake.

Pia taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani imeeleza kuwa kufuatia mamlaka aliyopewa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene kwa mujibu wa Sheria ya Uraia,Sura ya 357, (Rejeo la 2002) baada ya kupokea ombi lililoletwa kwake na TFF, amempa Uraia wa Tanzania mchezaji wa mpira wa miguu, Kibu Denis Prosper, Septemba 30,2021.


Kibu alikosekana kwenye mechi mbili za Simba ilikuwa mbele ya Biashara United na Dodoma Jiji.

13 COMMENTS:

  1. Kwake Kijana Haina shida hongera yake lkn wapendwa ndipo muone vituko vya Nchi hii.

    ReplyDelete
  2. Kuna binadamu wana roho mbaya, tukianza kuchunguzana mambo yatakuwa magumu, kuna watu sio raia pia wanajificha kwenye ufadhali na uongozi.

    ReplyDelete
  3. Kisa eti Yanga nao walikuwa wanahangaika kupata saini yake☹️

    ReplyDelete
  4. Kwa mtindo huu wa kutoa uraia kama njugu ipo siku mtatoa na kwa magaidi yatakayopitia kwa sura ya michezo.

    ReplyDelete
  5. nonsense jifuze kupitia ufaransa ureno na nataifa mengine ya ulaya

    ReplyDelete
  6. Pumbav wote fungeni midomo yenu humu .... Nimsikie sasa MTU anaongea fyongo humu ��

    ReplyDelete
  7. Jamaa sasa anaona aibu aende sasa akashauri jingine yaani mwaka huu ndiyo atakua hajui na awezi kushindana na mwenye pesa hapa dawa yake ni Kimuonyesha kuwa Hana jipya

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli watanzania hasa wale wanaosimamia michezo ubabaishaji je aliwezaje kuitumikia
    tanzania kwenye kimataifa Leo anafatiliwa na hao hao kwamba sio mtanzania kwakweli ubabaishaji wametuzoletesha Sana mechi tatu ngao ya jamii na mechi mbili za ligi kuu huu ulikuwa mpango wao tu hamna namna

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic