October 5, 2021


 BEKI wa kati wa Simba, Kennedy Juma, ameshonwa nyuzi sita baada ya kupata jeraha kubwa kwenye eneo la jicho kutokana na kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.

Kennedy alijikuta anaondolewa na machela kwenye uwanja dakika ya 43 ya mchezo huo kufuatia kupigwa na kiwiko na straika wa Dodoma, Anuar Jabir, ambaye naye alilimwa kadi nyekundu.

Mtu wa karibu na daktari wa Simba, Yassin Gembe, aliliambia Championi Jumatatu kuwa hali ya Kennedy inazidi kutengemaa na ameshonwa nyuzi sita jirani na jicho na kwa sasa anaendelea kuimarika.

“Kennedy jicho lilivimba kabisa, ile ilikuwa ni rafu mbaya sana ambayo alichezewa na yule mchezaji wa Dodoma, ililazimika ashonwe nyuzi sita ili kuweza kukaa sawa,” alisema mtu huyo.

Mtu huyo aliongeza kuwa Kennedy alilia na kusikitika sana baada ya kupata majeraha hayo kwa sababu alijua nafasi yake ya kwenda kambi ya timu ya Taifa imeingia mchanga.

“Kennedy alilia na kuumia sana moyoni kwa sababu hiki ndiyo kipindi ambacho alikuwa anaaminiwa timu ya Taifa Stars, sasa maumivu yake yalikuwa makubwa,".

Tayari nyota huyo kwa sasa anaendelea vizuri na alikuwa moja ya wachezaji wa Stars ambao walianza jana mazoezi na timu ya taifa ya Tanzania, Uwanja wa Mkapa.

6 COMMENTS:

  1. Hii ndio furaha ya watu wanaofurahia kuumizwa kwa wenzao kiasi mtu hadi anatoa hela kwa kazi hiyo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yule mchezaji wa aliempiga kiwiko Kennedy kwa makusudi sio wa kupewa kadi nyekundu tu ni wa kufungiwa mechi kadhaa za ligi pia kama fundisho na nitawashangaa bodi ya ligi kama wa watakaa kimya juu ya ukatili wa Anwari usio wa kimichezo.

      Delete
    2. Mkuki kwa nguruwe kwa Simba mchungu,pumbaaavu wakati Wawa anataka kumvunja mguu Nchimbi mlishanghilia hata pale Chama alipomtengua mguu Feisal pia mlihara leo kwa kuumizwa huyo msenge mnatoa povu.

      Delete
  2. Ni kitu kibaya sana kugeuza michezo kuwa uwanja wa vita

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe na Feisal Salum ni wahanga wa rafu za aina hiyo na zilikuwa zikishabikiwa waonyeni pia Lwanga na Bocco mpira sio vita

      Delete
  3. Afungiwe msimu wote wa mechi za round ya kwanza, maana tukilea huu ujinga kuna wachezaji watakuja kugeuka vipofu kwenye maisha yao, chonde chonde TFF msilee ujinga huu ambao cyo wa kiungwana kwenye michezo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic