October 8, 2021

 

MABOSI wa Manchester United wameambiwa kuwa itakuwa vema kwao ikiwa watapambana kupata saini ya kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya West Ham United,  Declan Rice.

Neno hilo limetoka kwa nyota wa zamani wa Arsenal wengi wanapenda kuwaita washika bunduki Nigel Winterburn ambaye amesema kuwa itakuwa sahihi ikiwa Manchester United watafanikiwa kupata saini ya nyota huyo.

Rice amekuwa akiwindwa na timu nyingi za Ulaya ikiwa ni pamoja na Manchester United, Manchester City pamoja na Chelsea ambazo zote zinashiriki Ligi Kuu England. 

Dau la kuipata saini ya kiungo huyo kutokana na ubora wake ndani ya uwanja linatajwa kuwa ni pauni milioni 90 jambo ambalo Nigel anaona kuwa itakuwa ni faida kwa United. 

"Pauni 90m ni fedha nyingi sana kwa ajili ya Declan Rice inashangaza ila huenda ni dau lake na atakuwa msaada kwa timu kama watampata,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic