October 14, 2021


KLABU ya Newcastle United inatajwa kuanza kuandaa orodha ya mastaa wakubwa ambao watakuwa ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Hivi karibuni klabu hiyo imenunuliwa na matajiri wakubwa akiwemo Mohammed bin Salman na Simon Brothers inaonyesha kuwa inataka kushusha majembe kadhaa ya maana kwenye ligi.

Kuna nyota kibao wakubwa wamekuwa wakitajwa kwamba wanaweza kuibuka katika kikosi hicho kutokana na uwepo wa mkwanja wa kutosha kwa mabosi hao wapya.

Mastaa ambao wanatajwa kuwekwa kwenye rada za timu hiyo ni pamoja na Gareth Bale, Edinson Cavani, Neymar Jr na Mauro Icard.

Pia jina la Steven Gerrad ambaye anaifundisha Rangers ya Scotland linatajwa kuwa kwenye orodha ya makocha ambao wanaweza kuinoa timu hiyo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic