October 1, 2021


 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wameambulia ushindi wa kwanza kwa msimu wa 2021/22 baada ya kuanza kwa sare katika mchezo wa kwanza walipocheza dhidi ya Biashara United.

Ikiwa Uwanja wa Jamhuri,ilipata ushindi kupitia nyota wao Meddie Kagere ambaye alianzia benchi.

Alipachika bao hilo dakika ya 69 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 na lilimshinda kipa wa Dodoma Jiji Hussein Masalanga na kuifanya Simba kusepa na pointi tatu.

Kushangilia kwa Kagere baada ya kuvua jezi kulimfanya mwamuzi amuonyeshe kadi ya njano.

Sasa Simba inafikisha pointi nne kwa kuwa mchezo wa kwanza ubao wa Uwanja wa Karume, Mara ulisoma BiasharaUnited 0-0 Simba.

Inafikisha pointi nne na kuwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza baada ya kucheza mechi mbili.

Dodoma Jiji walikamilisha dakika 90 wakiwa pungufu kwa kuwa nyota wao Anuary Jabir alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonekana akimchezea faulo Kenned Juma ambaye hakumaliza dakika 90.

6 COMMENTS:

  1. Mwandishi ni kama ameumizwa na ushindi wa simba, unaposema imeambulia una maanisha nini?

    ReplyDelete
  2. Anamaanisha ushindi wa jasho na damu

    ReplyDelete
  3. Ndio jasho liliwatoka si mchezo

    ReplyDelete
  4. Wewe umezoea kupata ushindi laini kwa kupitisha m pesa? Hizo hela mnazogawa kwa timu pinzani ili kuikamia simba si bora muwape wachezaji wenu?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic