October 1, 2021


 LEO imekuwa ni siku mbaya kazini kwa Biashara United baada ya kukubali kupoteza pointi tatu kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara mbele ya Ruvu Shooting wazee wa mpapaso.

Kipindi cha kwanza Wanajeshi hao wa mpakani waliweza kukazana na kulinda lango lao mbele ya Ruvu Shooting ambapo ubao ulisoma Biashara United 0-0 Ruvu Shooting.

Iliwachukua dakika mbili Ruvu Shooting kupachika bao la kuongoza na lilikuwa la ushindi kupitia kwa Rashid Juma ambaye alipachika bao hilo dakika ya 47.

Biashara United wamebainisha kuwa imekuwa siku mbaya kazini baada ya kupoteza pointi tatu jumlajula.

Kweye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara dhidi ya Simba, Biashara United walikomaa mbele ya Simba na kugawana pointi mojamoja.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Biashara United 0-0 Simba na kuwafanya watoshane nguvu na mabingwa watetezi.

Ruvu nao walikusanya kichapo kutoka Dodoma ambapo walionja joto ya jiwe kutoka kwa Dodoma Jiji kwa kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Cleophance Mkandala.

Leo Mkandala jitahada zake mbele ya Simba zilikwama kuipa ushindi timu yake kwa kuwa imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

7 COMMENTS:

  1. Tabu ya kukamia game kubwa ndo hiyo, hakuna mwendelezo wa matokeo mazuri.

    ReplyDelete
  2. Hii ndio faida ya kutumia nguvu zote kuizuia simba, leo hapakuwa na ahadi ya milioni 15? Kipigo mlistahili. Akija yanga mtaoewa 15m ili mufungwe, kenge nyinyi.

    ReplyDelete
  3. Hivi vitimu vidogo vinaharibu mpira wetu. Kazi yao ni kukamia Simba, Utopolo na Azam. Vikikutana vyenyewe kwa wenyewe vinatepeta kenge hawa

    ReplyDelete
  4. Makoro bado, ndio mujue mna benchi gani la makocha..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic