October 7, 2021

 


MCHEZO wa kuwania Kufuzu Kombe  La Dunia 2022 nchini Quartar,  timu ya taifa ya Tanzania imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Benin.


Kipindi cha kwanza Stars walikosa nafasi ya kupata bao la kuongoza kupitia kwa Simon Msuva ambaye aliweza kumkwepa kipa ila shuti lake liliokolewa na beki.


Mtupiaji wa bao leo Oktoba 7, Uwanja wa Mkapa ni Steve ambaye alipachika bao hilo dakika ya 71 kwa shuti kali akiwa nje ya 18.


Jitihada za Stars kupata bao zilikwama ambapo mshambuliaji John Bocco alikosa nafasi ya wazi akiwa ndani ya 18 kwa kushindwa kufunga baada ya shuti lake kuokolewa na kipa wa Benin.


Pia Stars ilikwama kutumia kona ambazo ilipata kipindi cha kwanza zilizokuwa zikipigwa kupitia kwa beki Israel Mwenda. 


Katika dakika 5 za mwisho kipindi cha pili Stars wakiwa nyuma kwa bao moja walijitahidi kufanya mashambulizi makali kupitia Abdul Suleiman, 'Sopu', Meshack Abraham na beki Bakari Mwamnyeto naye alifanya mashambulizi ila milango ilikuwa mgumu.


Ni mchezo wa kwanza Stars kupoteza katika kundi J na wanapoteza pointi tatu mazima ikiwa Uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wake.


Kwenye msimamo sasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne na vinara ni Benin wenye pointi 7.

4 COMMENTS:

  1. Kujiamini sana kumeiponza timu

    ReplyDelete
  2. SalehJembe muwe mnaweka updates wakati wa mechi za taifa, kama mnavyofanya za Simba na Yanga zikicheza, sio rahisi watu wote wanakua kwenye TV au Streaming muda wa match.

    ReplyDelete
  3. Taifa stars uwezo mdogo wachezaji wana papara kama hawajawahi kucheza mpira, forward butu, nilijua Kibu Dennis anaweza kufanya maajabu lkn anaishia kukaa na mpira mpaka anapotesa, team ina kwenda kushambulia mchezaji anapiga pasi za kurudi nyuma, kwakifupi hakuna team ya kwenda world cup pale. Ni kutiana pressure na aibu tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic