FT:Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Simba inasepa na pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji ikiwa ni mchezo wa pili kwenye ligi na wanakusanya pointi na kufunga bao kwa mara ya kwanza.
Kipindi cha pili
Dodoma Jiji 0-1 Simba
Zinaongezwa dakika 5
Dakika 90 Bwalya kwake Bocco ni zamu ya Dilunga anachezewa faulo
Dakika ya 89 Inonga kwake Bocco, Mzamiru kwake Bwalya kisha ni zamu ya Inonga kuelekea Dodoma Jiji ni Kibacha anaokoa majalo
Dakika ya 88 Mzamiru Yassin anafanya jaribio akiwa nje ya 18 lnakwenda juu ya lango
Dakika ya 87 Masalanga anaokoa hatari kwenye lango lake na kuanzisha kuelekea kwa Simba
Dakika ya 86, Dilunga kwake Meddie, Bwalya kwake Nyoni mlinda mlango Masalanga anainyaka
Dakika ya 84 Simba wanapeleka mashambulizi kwa Dodoma Jiji kupitia kwa Mugalu
Dakika ya 77 Manula anapewa huduma ya kwanza baada ya kuchezewa faulo na mchezaji wa Dodoma Jiji ambaye alionyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 69 Kagere anafunga goooooooal kwa pasi ya Mugalu ya kichwa akiwa ndani ya 18.
Dakika ya 63, Lwanga anatoka anaingia Kagere, anatoka Mhilu anaingia Duncan Nyoni, Tshabalala anafanya jaribio linaokolewa
Dakika ya 59 Salmin Hoza anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Lwanga
Dakika ya 58 Mkandala anapeleka mashambulizi kwa Simba inaokolewa na Manula
Dakika ya 57 Dodoma Jiji wanapeleka mashambulizi Simba
Dakika ya 56 Bocco anatoa mpira nje
Dakika ya 54 kona ya kwanza kwa Simba inapigwa na Bwalya
Dakika ya 52 Karihe anaingia anatoka Mcha, anafanya jaribio kali nje ya 18 linaokolewa na Manula karibu na Joseph Akamba ambaye ni mwamuzi wa kati
Dakika ya 51 Masalanga anaanzisha mashambulizi kwenda Simba
Dakika ya 50 Dodoma Jiji wanapeleka mashambulizi Simba, Inonga anaokoa
Dakika ya 46 Bocco anafanya jaribio la kwanza linakwenda juu ya lango
Dakika ya 45 John Bocco anaingia anatoka Mwenda
Kipindi cha pili kimeanza
Mapumziko
Dodoma Jiji 0-0 Simba
Dakika ya 45 Inonga anaingia anatoka Kenedy Juma
Dakika ya 44 Anuary Jabir anaonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Kenedy Juma
Dakika ya 40 Kenedy Juma anapewa huduma ya kwanza baada ya kugongana na mchezaji wa Dodoma Jiji
Uwanja wa Jamhuri, Dodoma
Dodoma Jiji 0-0 Simba
Dereva msaada kwenye tuta!!!!!!
ReplyDeleteMtateseka sana na ngoja tupate first eleven na huyo zeruzeru wenu,tunachukua mara tano mfululizo ili mjitoe vizuri kwenye league
ReplyDeleteMshapigwa changa la macho...hehehe
DeleteKikosi kipana kimekuwa cha kutafuta first eleven tena?
ReplyDeleteNashangaa!
DeleteMnatoa hela tuumiziwe wachezaji, huo ufala.
ReplyDeleteSafari hii hamna za kupenyeza sio? Wajitegemee ndio kazi yao.
DeleteSimba imepeleka wachezaji 9 kwenye timu ya Taifa, hilo linaonekana kuwaumiza wengine.
ReplyDeleteKwa viwango vya bongo..sisi tuko professional zaidi
DeleteProfessional ya nini labda??mngepigwa na rivers nje ndani??mnajitoa ufahamu mmepigwa jumla ya mechi tatu,zanaco,na mkapigwa na rivers kwa mkapa na mkapigwa tena nigeria,wakati simba kapigwa mechi mbili ambazo ni ya mtani na na mazembe ila ninyi mnajifanya kujitoa ufahamu kwelikweli poleni sana,endeleen kusubiri meli airport atashuka rubani utasema nahodha.poleni sana.
Delete