October 7, 2021

 


TIMU ya taifa ya Tanzania ya Wanawake, Twiga Stars imetinga hatua fainali katika michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini.


Leo Oktoba 7 imepenya hatua hiyo kwa ushindi wa penati 3-2 mbele ya timu ya Zambia baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.


Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa sababu timu zote zilikuwa hazijaruhusu nyavu zao kutikiswa.


Twiga Stars ilikuwa imefunga mabao 8 na leo imepachika la 9 huku Zambia ikiwa ilikuwa imetupia mabao 9 na leo imetupia bao la 10.


Katika mashindano hayo yalishirikisha timu 12 ambapo tatu ni Tanzania,  Uganda na Sudan Kusini ni wageni waalikwa.


Ushindi huo unaipa nafasi Twiga Stars kutinga hatua ya fainali ambapo inamsubiri mshindi wa fainali ya pili kati ya Afrika Kusini v Malawi.

3 COMMENTS:

  1. Hongera sana Twiga Stars!

    ReplyDelete
  2. Aisee wapo vzr sana, hii samia dream team

    ReplyDelete
  3. hongera zenu
    bora nyinyi ndo mngecheza na Benin maana kaka zenu wamezingua
    mechi ijayo wawakodi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic