BAKHRESA (KULIA), KUSHOTO KWAKE NI KAMGUNA, MMOJA WA WAJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA SIMBA. |
Mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Amin
Bakhresa ameibuka na kumtaka Michael Richard Wambura, kutoa ushahidi kuhusiana
na kashfa ya rushwa na rushwa ya
ngono.
“Hivyo tunataka atoe ushahidi, sisi tuko tayari na
kamati hii ina watu waadilifu sana, sasa kauli za kubahatisha za Wambura si
nzuri.
“Kama unakumbukam kamati hii ndiyo ilimpitisha Wambura
kugombea uchaguzi Simba kwa kuwa waliompinga hawakuwa na vielelezo.
“Kamati ya rufaa ya TFF ikamkata, nashangaa wakati
huo hakusema alitoa rushwa kupita.
“Sasa leo amekatwa baada ya waliokata rufaa kuwa
na vielelezo sahihi, ajabu anatutukana tena maneno makali sana.
“Hivyo akanushe au alete ushahidi, la sivyo
tutaenda mbele zaidi na kulifikisha sehemua ambayo suala hili litashughulikiwa,”
alisema Bakhresa.
Wambura alilaumu kwamba kuna rushwa inatembea kwa
lengo la kummaliza na kusema pia kuna rushwa ya ngono.
Wambura alienguliwa baada ya kuonekana uanachama
wake Simba ulisimamishwa baada ya yeye kwenda mahakamani kuishitahi klabu hiyo
mwaka 2010.
Tayari Wambura ambaye kundi lake limekuwa lile
linalofanya vurugu lukuki ingawa wengi wao wamebainika si wanachama Simba,
ameishakata rufaa TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment