June 1, 2014

MANJI

Milionea Yusuf Mehboo Manji, ataendelea kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga kwa mwaka mwingine mmoja.


Wanachama wa Yanga waliokutana leo kwenye makao makuu ya Ukumbi wa maofisa wa Polisi, Oyterbay jijini Dar es Salaam, wamefikia uamuzi huo.

Wanachama hao, waliamua kumpa Manji miaka minane lakini yeye akakataa katakata na mwisho akakubali mwaka mmoja tu.

Wanachama hao walikubali kwa pamoja, bila hata ya mmoja kupinga wakati zilipopigwa kura za ndiyo.

Mweyekiti wa Bodi ya wadhamini wa Yanga, Mama Karume alikuwepo na ndiye alianzisha hoja ya kutaka Manji aendelee kuongoza Yanga kwa miaka mingine nane.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic