September 16, 2014



Ronaldinho amekumbana na kitendo cha ubaguzi wa rangi kutoka kwa mwanasiasa mmoja nchini Mexco.
Mwanasiasa huyo kutoka chama cha PAN amembagua Ronaldinho akimfananisha na sokwe.

Sababu kubwa ya kumbagua ni kutokana na foleni kubwa ya magari barabarani iliyosababishwa na mashabiki wa timu ua Querétaro aliyojiunga nayo nchini Mexico.
Wengi walikuwa wanatokea uwanjani wakati Ronaldinho anatambulishwa.
Mwanasiasa huyo akaamua kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, kama anachukizwa na mchezo wa soka na anashangazwa watu kusababisha foleni sababu ya sokwe mmoja.
Kauli hiyo ilipingwa na wengi na kusababisha mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri kuifuta post yake.

Hata hivyo, watu wameendelea kumsakama na kupinga kitendo chake hicho cha kibaguzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic