January 11, 2015

Klabu ya Swansea imekubali kumuachia mshaambuliaji nyota, Wilfred Bony ajiunge na Manchester City.


Bony aliyefunga bao la nne wakati Ivory Coast ilipoifunga Taifa Stars mabao 4-2, Juma Kaseja akiwa langoni, sasa anaungana na Yaya Toure ambaye ni nyota wa Manchester City.

Swansea imekubali kumuachia Bony kwa kitita cha pauni milioni 30.

Lengo la Kocha Manuel Pellegrini ni kuwa na washambuliaji wanne ili kupambana na mikiki ya Ligi Kuu England.

Bony ndiye amekuwa akiaminika kama Drogba mpya katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic