Mchezo
wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika jana jumapili jijini Mwanza kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba kati ya wenyeji timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya
timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) umengiza jumla ya tsh 72.839,000 kutokana
na idadi ya washabiki 15,762 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Mgawanyo
wa mapato kwa mchezo hu ni VAT 18% sh. 11,111,103, gharama za tiketi sh.
3,203,700, gharama za mchezo (15%)sh. 8,778,639, Uwanja (15%) 8,778,639, CAF
(10%) sh. 5,852,426 na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF (35%) sh.
35,114,560.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini inatoa shukrani kwa chama cha soka mkoa wa Mwanza
(MZFA) kwa ushirikiano wao katika kufanikisha maandalizi ya mchezo huo,
waandishi na vyombo vya habari mbalimbali kwa sapoti waliyoitoa kwa timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
Aidha
TFF iinawashukru wapenzi, wadau na washabiki wa soka nchini, na hususani wa
kanda ya ziwa waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo, kwani
waliishangilia Taifa Stars tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho kwa ustaarabu wa
hali juu.
Katika
mchezo huo Taifa Star ilitoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya The Flames, bao la
wageni lilifungwa na Mecium Mhone kabla ya na Mbwana Samatta kuisawazishia
Tanzania.
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA.
0 COMMENTS:
Post a Comment