September 13, 2020


 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema hakuna mtu anayeweza kumuondoa kwenye timu hiyo kwa sasa.

 

Mo ambaye anafahamika kama mmoja kati ya mashabiki kindakindaki wa timu hiyo, amesema anaamini baada ya muda mchakato mzima wa uwekezaji utakamilika, lakini pamoja na watu kuwa wanazungumza mambo mengi, yeye hajali na hawezi kuondoka.


Akizungumza na Spoti Xtra jijini Dar es Salaam, bilionea huyo alisema kuwa anaamini asilimia kubwa ya watu wa Simba wanampenda na yeye ana nia njema na timu hiyo, hivyo hatishiki na wachache ambao wanampiga vita.

 

“Kuna mambo mengi sana yanaendelea, lakini jambo la msingi ni kwamba sina mpango wa kuondoka kwenye timu hii kwa sasa.

 

“Naamini kuwa kuna watu wana maneno yao, lakini wale wa Simba bado wananiunga mkono na wanataka niendelee kukaa hapa, nami napenda kuwaambia kuwa nipo na nitaendelea kuwepo labda hao wenye Simba yao waniondoe, lakini mimi siwezi kuondoka hata siku moja,” alisema.

 

Mo amesema kuhusu uwezo wa mtendaji mpya wa timu hiyo, Barbara Gonzalez na anaamini kuwa atafanya kazi nzuri kwa kuwa alipitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na siyo yeye kama inavyodaiwa.

 

“Barbara amekuwa chini ya Senzo Mazingisa (CEO aliyepita), kwa kipindi chote na amefanya kazi nzuri, mimi naamini ataendelea kufanya kazi nzuri na watu wanatakiwa kufahamu siyo mimi niliyempitisha kuwa CEO bali ni Bodi, kila mmoja alisema anafaa kwa kuwa wanamuamini,” alisema Mo.

32 COMMENTS:

  1. Utaondoka tu! Hujatoa hela unaongoza timu kama nani? Unajaza watu wako kwenye uongozi wakati una hisa chache (asilimia 49 tu na bado hujazilipia). Utaondoka tu. Kwa sasa wewe ni mwanachama tu kama wanachama wengine. Usijipe mamlaka ya kufanya maamuzi klabuni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yeye ndiyo mwenye hisa nyingi 49, hizo nyingine zinakuwa kwa wengi, tuletee wewe mwenye hisa nyingi zilizolipiwa. Kwenye mfumo wa hisa mwenye hisa nyingi pia anakuwa na maamuzi makubwa.

      Delete
    2. Lakini kwa nini sasa hataki kuzilipia na timu kashaichukua mapato yote yapo chini yake? Mkataba wake wa uwekezaji ulimtaka alipe asilimia 30 siku aliyeshinda tender ya kuwa mwemezi. Kwa nini anavunja makubaliano kwa makusudi. Sasa yeye anasimama nafasi gani kwenye hii simba bila kutekeleza chochote?

      Delete
    3. Kinachoshangaza akiulizwa anakuwa mkali

      Delete
    4. Ukweli ni kwamba unaweza kuwafanya watu wote wajinga lakini huwezi kuwafanya wote kwa wakati mmoja

      Delete
    5. Eti utaondoka tu, mara nyani mwingine kakurupuka eti akiulizwa anakuwa mkali, eeh mara kaja tumbili eti ukweli ni kwamba unaweza kuwafanya watu wote wajinga lakini huwezi kuwafanya wote kwa wakati mmoja nyie manyani mmeshachangia shilingi ngapi pale simba mrudishiwe pesa zenu YANI MANYANI WANAJIFANYA WANA UCHUNGU NA SIMBA KUMBE ROHO TU NDO ZINAZOWAUMA VUMILIENI KIDOGO LABDA MPAKA MWAKA 2025 tutawachia kidogo na nyinyi mjifariji

      Delete
    6. Mo haondoki simba yupo kisheria.
      Wanaosema Mo aondoke ni wa utopolo fc.
      Yanga kama kuna amchezaji pale simba wanaemuhofu na kutamani aondoke basi ni mchezaji wa 12, wa kikosi cha simba ambae ni Mo. Hata hizi comments za kusema Mo aondoke ni za wana makasu makasu wa jangwani.
      Kwani yule GSM injinia saidi yupo yanga kama nani? Kashindwa kumzuia Morrison kuondoka halafu anawapiga changa la macho kwa kusajili wachoma mahindi wa vita wanakuja hapa wanabebwa kama wafalme.Mfalme kwenye soka la bongo mpaka sasa ni mmoja tu nae ni Mo. Yanga kama wangempata tajiri kama Mo hata hizo billion ishirini asingeambiwa atoe,wangempa timu bure na jina la tmu wangebadilisha na kuita Mo yanga Africans. Acheni choko choko Mo hang'oki sumba na kama manataka kuling'oa soka la Tanzania hapa lilipofikia basi mng'oweni Mo pale simba. Kingwala ajitafakari kwani anaanza kutitia hofu watanzania kwani asije akaanza kukata vitalu vya mbuga zetu kulipia piki piki. Watanzania wanapaswa kumshukuru Mo kwa kukataa kumuhonga mmoja wa mtumishi wetu nyeti sana anaesimamia rasilimali zetu za taifa kwani kama Mo asingekuwa mzalendo angetoa tu pikipiki na kujua jinsi ya kulipana.

      Delete
  2. Replies
    1. Yote haya ni draw ya jana na Mtibwa. Mechi ijayo atawanunulia mechi washinde wiki Watakaa kimya ameshawajulia

      Delete
    2. Kweli aisee, mbumbumbu wakifurah wanasahau

      Delete
    3. Kweli aisee, mbumbumbu wakifurah wanasahau

      Delete
    4. Ni heri mbumbumbu unaweza kumuelimisha akaelimika kuliko Matahira fc ambayo yanaongopewa kuwa wamevunja mikataba ya wachezaji yanaenda kuganda Uwanja wa ndege kupokea magarasa yaliochwa na AS VITA na kwa sababu ni matahira yanambeba yule kiongozi wao kwa ishara za kitumwa yani Tahira si hajui lolote kwa hiyo yenyewe yanaona sawa, alafu yanapiga kelele GSM GSM GSM jamaa anawacheka anaona kweli haya ni matahira ambayo hata Milembe kwenyewe wameyataa kwa sababu hayawezi kupona labda kwa miujiza tu

      Delete
  3. Alipe pesa sio akiulizwa anakuwa mkali mara oh nimeshaongelea wasafi fm hivi unaongea na kitenge na zembwela ndio wanasimba

    ReplyDelete
  4. Aha aha aha yani ukisoma hizi comment ndo utajua Tanzania kwa nini inabidi tufanye re shuffle ya elimu yetu kuanzia chekechea mpaka chuo, maana naona bado wapumbavu ni wengi sana maana bora mjinga unaweza kumuelimisha akaelewa lakini mpumbavu ni yule ambaye hata ukimuelimisha muda mwingine anajitoa mpaka ufahamu, yani mtu anachokiandika unaona kabisa hakuna chochote anachokijua wengine ni washabiki wa Manyani fc wamechukizwa na kauli ya Mo kwamba siwezi kuondoka simba, maana matumaini yao yakuona simba ikirudi kule ilipotoka yameyeyuka masikini utopolo baada ya simba kutoa droo jana wamepata la kuongea lakini ligi inaendelea mkumbuke walipotufunga lile goli lao moja la kichawi waliona dunia yote ya kwao kilchofuata wote tunajua wamebomoa timu nzima, Alafu wewe unayeitwa siju Rodrick wewe sio mshabiki wa simba bali kidampa mmoja tu ambaye sidhani hata kama mpira wenyewe unaujua, sidhani hata kama unajua gharama za uendeshaji wa timu, na nyinyi ndo wale wale hata hiyo bilioni ishirini ikiwekwa mtatoa sababu nyingine mbona ela zenyewe zina rangi ya njano. MAGUFULI TUNAOMBA USIMAMIE KWENYE SUALA ZIMA LA ELIMU TANZANIA WENGI WAO WAMESOMA KWA AJILI YA KUHESABU ELA TU LAKINI UPUMBAVU UPO PALE PALE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe usijilinganishe na mimi nyie ndio walewale hivi ulielewa hoja ya kigwangala au ulisikia nini alisema jaji Mihayo alipohojiwa juu ya Mo kulipa share.
      Hivi unafahamu mo kanunua makampuni mangapi na mashamba ya serikali na nini alifanya au unajua kwanini mo alinyang'anywa mashama na serikali kama hujui nataka nikueleze halafu tuone mimi na wewe nani nani anah elimu.
      Mashamba ya mkonge alikopa benki na akaendeleza sehemu ndogo ndio maana akanyang'anywa.
      Uwekezaji wa Simba alitakiwa alipe asilimia kumi ndani ya mwezi mmoja na pesa yote baada ya miezi mitatu.
      Wakati Mkwabi akihoji juuvya kuweka bilioni 20 alikuwa anakimbia tweeter na kumpiga vijembe.
      Aliyeongoza mchakato alikuwa jaji Mihayo lakini alipoulizwa akasema wao walishamaliza sehemu yao iliyobaki ni sehemu ya viongozi kwa lugha nyingine wanaopaswa kufatiliwa ulipaji wa bilioni 20 ni viongozi waliochaguliwa.
      Kabla ya kutaka kuwekeza Simba alisema akishalipwa hizo pesa zingewekwa kwenye akaunti maalumu na faida ambayo ingepatikana ingetumika kwa ajili ya uendeshaji wa klabu lakini baada ya kukubaliwa kuwa mwekezaji akakimbilia kutaka hati ya jengo wakati halikuhusiana kama ameweza kujenga uwanja, kusajili timu na kulipa mishahara nini kinamzuia kuweka bilioni 20 na kama mchakato haujakamilika kwanini awe na maamuzi mazito.
      Kuna kipindi alikuwa anatangaza pikipiki za boxer kwenye mechi za simba wakati haipo kwenye mkataba, kwenye simba say alitanga sabuni ya mo protector wakati haipo kwenye mkataba ndio maana wakahoji kuteua msaidizi wake kuwa ceo wa simba hakutakuwa nammgongano wa kimasilahi kati ya simba sa kampuni zake.
      Hakuna anayepinga uwekezaji simba ila mo aache janiajanja jina lake limewekwa kwenye viwanja vya simba hivi unajua arsenal inalipwa shilingi ngapi kwa uwanja wao kuitwa Emirates halafu unakuja hapa kujifanya una elimu kumbe ngumbaru fulani ambaye hujui abc za hisa wala uwekezaji.

      Delete
  5. Hivi nikuulize swali huyo Kigwangala wewe unayesema ana hoja hivi angekuwa ni mshabiki wa simba anayesema yeye ni simba kindaki kindaki, suala la uwekezaji wa Mo la bilioni ishirini angeenda kuhoji tweeter kwa nini kwanza asingetafuta wahusika awahoji na majibu yasingejitosheleza angetafuta njia nyingine alafu ishu ya Mo sijui kukopa mashamba ya Serikali inahusiana vipi na uwekezaji wake ndani ya simba kama Seruikali ya magufuli ingekuwa inajua huyu mtu ni mbabaishaji ingeweza vp kumkubalia aendelee na mchakato wa uwekezaji pale simba,l alafu ishu nyingine inayoniaminisha kwamba wewe ni mkurupukaji kama kigwangala unasema Mo alikuwa anatangaza piki piki zake Boxer uwo ni uwongo, na hao Mo protector unaowasema wana mkataba wa kihalali na simba na hayo maamuzi unayosema wewe mazito Mo hajawahi kufanya uamuzi wake binafsi bali bodi ya wakurugenzi ya simba huwa inakaa na kufanya maamuzi hata uteuzi wa CEO ni bodi ndo imekaa ikaridhia kwamba Barbara Gonzalenz awe CEO mpya wa simba, na kama mchakato wa kuweka Bilioni ishirini ungekuwa umekamilka kuna mamlaka za Serikali zingepaswa kumuhoji Mo kwanini hajaweka hizo pesa kwa hiyo wewe unaonekana ni bendera mfuata upepo hao wanao hoji zilipo bilioni ishirini si ndio hao hao waliokuwa wazuia hati, leo hii zikiwekwa bilioni ishirini mtakuja na sababu nyingine mbona ela zenyewe ni za kijani. Na kwa taarifa yako hiyo sijui asilimia kumi unayoisema angeweza kuweka na kukaa pembeni akwaambia wanachama mpaka wamalize mchakato wote upande wa silimia 51 ikiwepo ukaguzi wa hesabu za simba tangu mwaka 2015 alafu yeye ndipo atatoa hizo bilioni ishirini lakini Mo kwa mapenzi yake kwa simba anatoa bilioni mbili kila mwaka ili ku boost bajeti ya simba ambayo sasa hivi imefikia bilioni 7 kwa mwaka kutoka muilioni 400 mwaka 2015, sasa wewe unazungumzia asilimia 10 ambayo ni bilioni 2 muda wmingine msipende kufuatisha mkumbo kwa kila mnachokisikia, alafu kitu kingine wewe unahoji kuhusu bilioni ishirini na huyo kigwangala wako umeshawahi kujiuliza Mo akiweka hiyo b. 20, na upande wa silimia 51 umeshaweka shilingi ngapi? usipende kufuata mkumbo kwa kila unachokiona kwenye mitandao ya kijamii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Napenda unavyojitahidi kujibu hoja bila kukimbilia kusema eti hawa Wajinga. Kusome vzr makubaliano ndugu yangu wewe ni mwanasimba. Mtaji asilimia 51 wa wanachama hawatakiwi kutoa fedha. Ni mali za Simba SC na wanachama. Hivi watu mnakaa mnakubaliana atakae shinda huu mchakato atoe 10% ndani ya mwezi arafu mtu hatoi. Hii ni nini? Badala yake jezi ya Simba leo imejaa matangazo kila kona mara sabuni, Mafuta, Juice nk. Kwa hiyo wanasimba wote tumtangazie biashara wakati yeye hajatoa ata shilingi?

      Delete
    2. Tatizo watu wakihoji mambo ya msingi watu wanakimbilia nje ya mada.Mo kaingia mkataba wa uwekezaji huo mkataba uko kisheria cha muhimu ni kila pande kuheshimu makubaliano waliyoingia kama makubaliano alipe pesa baada ya miezi mitatu alipe kama mchakato haujakamilika waite mkutano waeleze nini kinakwamisha na sio kukimbilia kuwasema wanahooji bilioni 20 .pia mo asikimbilie kutoa ruzuku badala yake asikimbilie kusema analipa mishahara au kujenga uwanja anatakiwa kujua alichotakiwa kutoa ni bilioni 20 kwa sababu kuna bodi wao na bodi wangekaa kuamua namna wangwekeza hizo pesa
      Sasa kuna watu hawajui hisa ni nini ndio maana wengine wanauliza hisa za asilimia 51 mbona hawajaweka pesa nashukuru umesaidia kumuelewesha huyo jamaa

      Delete
    3. Kwa hiyo wewe kwa akili yako ya kawaida pesa aliyotumia Mo mpaka sasa, na hiyo asilimia 10 unayoisema wewe ambayo ni bilioni mbili zinalingana, yani kila mkiambiwa mchakato wa kuweka bilioni ishirini haujakamilika na wanaokwamisha mchakato huo ni upande wa wanachama kwa sababu kuna vitu wakati mchakato ukiwa unaendela hawakuvijua mfano UKaguzi wa hesabu simba kuanzia mwaka 2015 mapaka 2019 hazipo upande wa wanachama unabidi uwasilishe na kwa sababu hivi vilabu vyetu vilikuwa vinaendeshwa kiujanjaujanja ndio mana hata hizo hesabu inachukua muda mrefu kuwasilishwa lakini watu wanang'ang'ania tu bilioni ishirini mbona haijawekwa

      Delete
  6. Watu mnashindwa kuelewa kitu kimoja tu, hayo matangazo yote mnayo yaona hao ni wadhamini wa simba jamani na simba wanapata zaidi ya milioni mia nne(milioni 400) kutoka kwa hao wadhamini wame risk kuidhamini simba, shida ni kwamba watu wanafikiri hayo matangazo ya Mo protector , Mo juice yapo pale bure tu kwa sababu Mo yupo simba hapana huo si ukweli,wale ni wadhamini kama unavyoona SPORTS PESA, leo hii yanga kwenye jezi zao kuna chapa ya GSM, Taifa Gesi hao ni wadhamini tuseme basi mbona hao GSM hata mchakato wa mabadiliko yanga haujaanza mbona kuna matangazo yao kwenye jezi ya Yanga. Yani sisi simba tumepata bahati ya Mwekezaji ambaye pia ana mapenzi na timu tusipoelewa hapo wanasimba hatutaelewa tena, na watu wengi wanaoshikia bango hii ishu ni washabiki wa Yanga ambao wao wanataka simba wavurugane alafu wao mambo yao yaende kwa sababu kwa hali ilivyo sasa ni vigumu kwa wao kushindana na simba Simba ndio timu inayozungumzwa sana Africa Mashariki na kati kwa sasa hilo linawauma wapinzani wetu na hii yote ni Mo amechangia kwa kiasi kikubwa na ndoto za Mo ni kuona simba inakuwa Klabu kubwa barani Africa muda mwingine tusipende tu kulaumu, Ujenzi wa Uwanja,ulipaji wa mishahara wachezaji, GPS System iliyofungwa ili kuwa monitor wachezaji, Recovery Center kwa ajili ya wachezaji yote hayo Mo anafanya nnje ya bilioni ishirini yani tuna shindwa kumpongeza hata kwa hili jamani muda mwingine muwe mna think twice.

    ReplyDelete
  7. Mo aelewe kwamba kukaa kimya siyo kumaliza Hoja. Anaweza kuwanyamazisha watu wote wanaohoji zilipo pesa za ununuzi wa 49% ya hisa (= 21bn) lkn ukweli utabaki na siku moja mawe yatapiga kelele. Suluhisho analijua, angetoa hizo pesa kisha walazi "ring fence" hadi wamalize masuala madogo yaliyobaki. Kufanya ukaguzi wa mahesaby ya Simba kwa miaka 5 iliyopita na utamini wa mali za Simba hauwezi kuchukua miaka 3!
    Mo acha maneno weka muziki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizo pesa hazitumiki Kama hivyo unavyo waza ww mwenye ufahamu mdogo kuhusu huu mfumo wa hisa mo. Hii 20 billion Ni Kama mtaji wa kuzalisga pesa nyingi zaidi ndani ya klabu nakuwa inayojitegemea kwa kila kitu idara zote.mfano: unachukuwa 19 milioni tunawejeza Vodacom, 20 milioni tunawekeza Nmb, 40 milontunawekeza tigo n.k na mwisho wa siku kila mwezi tutakuwa tunavuna mikwanja kutoka kwenye hizi taasisi na kufanya maendeleo ndani ya klabu. Wenye akili ndogo Kama zako wanawaza kwamba team itsgawana hizo pesa wakapige mzinga. Utopolo nendeni mkasome muelimike hata angakau QT tu.

      Delete
  8. Unatoaje tu pesa na mchakato haujakamilika mbona tunakuwa na vichwa vigumu sana kuelewa, bilioni ishirini siyo pesa tu pekee inayoweza kuifanya simba kuwa klabu kubwa barani Afrika, wanachama na washabiki kwa upande wao wanasapoti vipi kuifanya simba ipanuke kiuchumi je wananunua zile kadi za Simba za equity, wananunua jezi sio tunapiga kelele tu hapa bilioni ishirini wakati Klabu kama Pyramids wananunua mchezaji mmoja tu kwa bilioni 10

    ReplyDelete
  9. Mo alielewa kila kitu kabla hata mchakato haujaanza.
    Hivi mnakumbuka alivyokuwa mkali pale Simba ilipoingia mkataba na sportpesa.Hakuna pesa ya bure kama mahesabu au nini ninio vitu vilitakiwa kufanywa kabla ya mchakato lakini maneno yote yanayosikika ni kwa sababu mchakato ulifanywa kijanjajanja kwani yeye ndio alitamka bei tena ilikuwa asilimia 51 baada ya serikali kusema vilabu vinaruhusiwa kuuza asilimia si zaidi ya 49 akapewa kwa bei hiyohiyo ya asilimia 51 kama mkutano mkuu ulishamuidhinisha na bodi ikaundwa nini kinamzuia asitoe bilioni 20 na akihojiwa anakuwa mkali

    ReplyDelete
  10. Mimi ningekuwa mshauri wa Mo ningemshauri tu ajiondokee alafu tuwaone hawa wanaojifanya washabiki wa simba ambao wana uchungu sana na hii timu ambao inawezekana hata jezi tu ya simba hawana, wataifanyia nini simba yani we mjomba hapo juu unaonekana hata redio unaweza kubishana nayo na sina imani kama wewe ni mshabiki wa simba wewe utakuwa ni kibaraka wa GSM nimefuatilia comment zako unaonekana huna hoja yani we unataka bilioni ishirini ziwekwe tu bila kufuata utaratibu wa kisheria kama taratibu zote za kisheria zimefuatwa na mamlaka zinajua kwa nini sasa wao wasimwambie Mo anapaswa kuweka bilioni ishirini lakini wewe kidampa tu ambaye hujui chochote una nga'ang'ania ziwekwe bilioni Mo hajaichukua simba kama unayoenda sokoni kununua Nyanya kuna mamlaka za Serikali na zinajua hili swala mbona hatuwasikii wao wakihoji ila nyinyi vidampa ndio mnapaza sana sauti

    ReplyDelete
  11. Huyo asikuumize kichwa huyo ni mshabiki wa Yanga anyejifanya yeye ni simba mwenye uchungu kumbe nia yake aone simba inaharibikiwa, alafu stress zao ziishe mtaendela kuteseka sana

    ReplyDelete
  12. Asanteni sana kwa michango mizuri ya hoja. hii ndio ukisoma comments za wenzetu nchi zilizoendelea unakuwa wa kujenga. mara nyingi matusi hupigwa vita sana. utani unaruhusiwa.

    ReplyDelete
  13. Endeleeni kuongopewa hivyo hivyo na magazeti ya bongo

    ReplyDelete
  14. Mo kama Usajili na matumizi hayo mengine no sehemu ya Uwekezaji pasua jipu ,cse ukimpata mwanamke aliye kukubali mkaenda dinner gharama zote unazoingia ni sehemu ya kukubali wito hata ukisha mgosha hukampa kifuta jasho nauli nk hiyo ni sehemu ya matumizi ya Dinner.Simba wowowo toeni mzigo jamaa ameisha lipia Hotel.Kwani hizo pesa anazotoa anaokota?

    ReplyDelete
  15. Ila wewe unayetishia watu na Elimu waulize wote wanaotaja Yanga humu Elimu yao.Ugombane mkeo kwa fumanizi?usingizie jirani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic