January 21, 2021

 


JINA la kiungo mkabaji wa Klabu ya Simba, Taddeo Lwanga limeondolewa katika orodha ya wachezaji waliosajiliwa na Simba ndani ya kipindi cha dirisha dogo na kukabidhiwa kwa Shirikisho la soka Tanzania TFF.kwa ajili ya kutumika katika mzunguko wa pili wa ligi.

Lwanga alitambulishwa rasmi na Simba Desemba 2, mwaka jana kama sehemu ya mbadala wa Mbrazili, Gerson Fraga na kukaa nje kwa muda mrefu kabla ya kupewa nafasi kwenye michezo ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika mapema Januari mwaka huu.


Simba  imewasilisha majina mawili pekee kama sehemu ya wachezaji waliowasajili ndani ya kipindi cha usajili wa dirisha dogo, majina hayo ni; Tatenda Perfect Chikwende raia wa Zimbabwe na Mkongomani Doxa Gikanji.

 

Chikwende ametokea ndani ya kikosi cha FC Platinum huku Gikanji yeye akiwa ametokea ndani ya kikosi cha DC Motema Pembe.


Kwenye Kombe la Mapinduzi, Lwanga aliweza kucheza pia mechi kubwa ambayo iliwahusisha watani wa jadi kwenye fainali dhidi Yanga.

Aliweza kuyeyusha dakika zote 90 na kushuhudia timu yake ikifungwa kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.


13 COMMENTS:

  1. Mm kwa upande wangu sijaona lolote kuhusu huyo luwanga hakuna mcjezaji hapo

    ReplyDelete
  2. KUNA HARUFU YA "MCHEZO MCHAFU" BAINA YA TFF NA SIMBA SC KWENYE DIRISHA LA USAJILI KWA KUCHOMEKA WACHEZAJI NA KUNYOFOA WACHEZAJI "KIENYEJI" KINYUME NA KANUNI DIRISHA LA USAJILI MDOGO LILIFUNGWA TAREHE 15...SASA KUNA KINACHOENDELEA MARA LWANGA MARA CHIKWENDE MARA KAHATA MARA DOXA....TAKUKURU INGILIENI HAPA KUFUATILIA NYENDO ZA TAASISI NA MAHUSIANO YAKE NA SIMBA SC

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kumbuka Simba wanaruhusiwa kusajili wachezaji wa kuwasaidia katika michezo ya CAF. CAF walitoa hadi tarehe 30.01 na timu zilizofuzu makundi wanaruhusiwa kuongeza wachezaji 10 na hivyo kuwa na wachezaji 40 badala ya 30

      Delete
    2. Hama rushwa kipindi cha kusajili unaruhusiwa kuacha unaotaka kuwaacha na kusajili unaowataka. Jina last lwanga lilitakiwa kuingia kwenye orodha ya wachezaji wapya safari hii halijaonekana badala yake doxa ameingia hivyo lwanga atacheza kimataifa. Ligi ya ndani ushapata orodha tayari lwanga out, kimataifa lwanga in.

      Delete
    3. Hamna rushwa hapo ikumbukwe kipindi cha kusajili unaruhusiwa kuacha unaotaka kuwaacha na kusajili unaowataka. Jina la lwanga lilitakiwa kuingia kwenye orodha ya wachezaji wapya kwa marathon ya kwanza safari hii, lakini halijaonekana badala yake doxa ameingia hivyo lwanga atacheza kimataifa. Ligi ya ndani ushapata orodha tayari lwanga out, kimataifa lwanga in.

      Delete
    4. Kutokufuatilia mambo kunakufanya uonekane shabiki maandazi..Lwanga anacheza kimataifa. Tatizo lako kwa sababu Lwanga ina kaufanano na Yanga basi unachanganyikiwa coz hampo ��������

      Delete
  3. Mashindano ya CAF kanuni zake tofauti na za TFF, kuruhusiwa kucheza CAF haina maana wanaweza cheza Tz pia, kwamujibu wa TFF wanahitajika wachezaji 10 tu wakigeni, ndio maana unaona chomeka chomeka kienyeji mpaka nje ya dirisha la usajili

    ReplyDelete
  4. Sisi tunashiriki michuano ya KLABU BINGWA CAF CL na hilo tunaliangalia zaidi hatukai kuwaza VPL tu tunawaza yaliyo mbele yetu.
    Maana wengine wamekaa kupiga domo kwa kuona wivu tu na si vinginevyo.
    This Is SIMBA SPORTS CLUB.

    ReplyDelete
  5. Mpira wa tz bna,,,hayo yote yanaendelea bila kocha daaa,,,kocha akija akiwapiga benchi maneno kibao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Matola ndio kocha wetu. Tulia

      Delete
    2. Ligi imesimama, mashindano kimataifa bafo mchakato wa kupatikana kocha fuatilia kwa karibu. Unateseka ukiwa wapi???.

      Delete
    3. Karibu kocha mpya Simba tuendeeleze Moto achana na mabingwa wa mashindano ya m 15

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic