ALIYEKUWA Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara leo Agosti 24 ametambulishwa ndani ya Yanga kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.
Manara ambaye alikuwa ndani ya Simba kwa muda wa zaidi ya miaka 7 akitumikia kwenye nafasi ya Mkuu wa Kitengo cha Habari ameweka wazi kwamba atafanya kazi kwa ushirikiano na viongozi ambao amewakuta ndani ya Yanga.
Kuelekea kwenye Wiki ya Mwananchi inayotarajiwa kufika kilele Agosti 29, Uwanja wa Mkapa ameweka wazi kwamba atafanya mambo makubwa.
Pia ameongeza kuwa kazi anaanza kesho rasmi kwa kuzindua jezi mpya ambayo haina makando na itakuwa ni namba moja kwa ubora.
Utambulisho wa Haji Manara umefanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Serena katika mkutano wa Waandishi wa Habari ulioanza saa 12:58 jioni.
Akimtambulishwa na Senzo Mbatha ambaye ni Mshauri Mkuu kuelekea masuala ya mabadiliko amesema kuwa anarejea nyumbani na atafanya kazi kwa ushirikiano na wengine.
"Tunamtambulisha kwenu kwenye utawala mpya na anarudi kwa ajili ya kufanya kazi ndani ya Yanga. Anajua jukumu lake na anarejea nyumbani," .
Pole zake!!!!! Wape salaamu!!!!
ReplyDeleteKatika suala la Manara simba Kama Wana nafasi ya kumjengea sanamu lake Barbara basi wafanye hivyo haraka tu.Barbara yupo makini Sana kiasi Cha kumtambua Manara mapema tu kuwa sie.
DeleteKama kuna Wanasimba waliokuwa wakishindwa kumuelewa MADAM BARBARA GONZALE katika suala la KHAJI MANARA na tuhuma za kinafiki za Manara zidi yake sasa Manara amewajibu yeye mwenyewe kuwa Barbara hakuwa akimuonea au kumsingizia bali Barbara alikuwa yupo sahihi asilimia 100.
DeleteBarbara yupo vizuri na simba wanapaswa kujivunia kuwa na kiongozi kama yeye.
Yanga ni muendelezo wa kuwapumbaza mashabiki wao. Manara alikuwa atambulishwe siku ya mwanachi ila baada ya uongozi kushindwa kujitetea na kitendo Cha kuipeleka timu Morocco kutalii kwa siku nne 4 ndio wakaja na hili la Manara ili kufunika uozo wa preseason hewa ya Morocco.
DeleteAliwaita Utopolo sasa yeye amekuwa TOPOLO!!!!
ReplyDeleteHaha wanawachukua waliofukuzwa kwanza senzo sasa manara na manara simba damu aliwaita utopolo sasa yeye kawa matope
ReplyDeleteBora amehamia huko alikokuwa anapeleka siri za simba. Ila nashangaa anapewa jezi kwani anacheza namba ngapi? Au kapewa cheo cha uhamasishaji au usemaji?
ReplyDeleteSenzo na manara ni zaid ya brandy in footbollo
ReplyDeleteFootbollo. Manara utopolo
DeleteKilio cha mkosajiiii.. ngoja tuone mikia day ya anayekimbia kamwagwa na Barbara wenu...hehehe
ReplyDeleteUtamtambua kwamatendo
ReplyDeleteRasmi alikuwa anatuhujumu Simba hongera babra,hongera MO
Mpelekeni mirembe, hakika nati zimelegea
ReplyDeleteKenge wote babra endelea kuwatoa wabaki mamba tu hao kenge wanagaribu poozi
Mwaka huu mo atasajiriwa na GSM Hahah
ReplyDeleteKweli pale bado Mo,na Barbara.Lkn inauma
ReplyDeleteWewe kweli hamnazo unadhani MO ni manji yule
DeleteAISEE WANAFIKI DUNIANI NI WATU WAGUMU SANA KUWAJUA! SIKUTARAJIA KAMA MANARA HUYU ALIYEATUKANA YANGA LEO HII ATAKUWA YANGA DAMU
ReplyDeleteWatu wamehama Chadema na CCM sembuse kwa Wala dengu mikia!!!!???
ReplyDelete