KIKOSI cha Yanga, leo Septemba 13 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Bao pekee la ushindi lilipachikwa kimiani na beki kisiki wa Yanga, raia wa Ghana, Lamine Moro dakika ya 86 kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Carlos Carlinhos ambaye aliingia dakika ya 60 akichukua nafasi ya Feisal Salum.
Kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa, timu zote mbili zilitoshana nguvu ambapo zilikwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguzo zikiwa hazijafungana.
Kipindi cha pili pia ushindani ulikuwa mkubwa ambapo Yanga iliweza kufanya mabadiliko ya wachezaji wake watatu ikiwa ni pamoja na Deus Kaseke ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Yacouba Sogne pamoja na Haruna Niyonzima ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Ditram Nchimbi.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi nne kibindoni baada ya kucheza mechi mbili huku Mbeya City ikiwa na haijavuna pointi kwenye mechi zake mbili ilizocheza na imefungwa jumla ya mabao matano.
Mchezo wa kwanza ilifungwa mabao 4-0 mbele ya KMC na imepoteza pia mchezo wake wa pili mbele ya Yanga.
Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 19, Uwanja wa Kaitaba.
Leo suluhu yanga, tuna kwama wapi
ReplyDeleteSema wewe unakwama wapi?
ReplyDeleteTimu mbovu sana. Mimi Yanga lakini kwa mpira huu hatufiki popote.
ReplyDeleteKMC Ni Bora kuliko utopolo
ReplyDeleteTukicheza NYUMBANI hivi.Tukianza kwenda mikoani itakuaje?
ReplyDeleteWiki ijayo na Kagera lazima tubadilike au Kaitaba tutaadhirika.
Utopolo msiwe na wasiwasi refa mpeni pamper (jezi ) mtashinda na kagera
ReplyDeleteTimu zote ni nzuri sana tuwe na matumaini wenzangu
ReplyDeleteWewe mkia Mtibwa kaukunja , utadhani mbeya city walitaka maana kila faulo wanalala chali,wewe kuwa Yanga au kutokuwa Yanga siyo sababu ya kujifanya eti hatufiki popote .wenye marefa jana umeona .Leo refa kuwasaidia sana mbeya city Sana bila kusahau bange walolishwa na mikia kupitia Amri Said chaaaali hope mmemwona mdogo wake de bruyne Bongo leo pasi na free kiki za viwango hao Watoto Mbeya City wanahitaji mapumziko ya mwezi maana wote wameumia waulize Prison walikaza povu hilo Jana na KMC majeruhi wote .Hiyo ndo dawa ya mabange mlowapa wakaze .Kimoko tu wanalia
ReplyDeleteWape salaam
DeleteMpira hauchezwi mdomoni wala magazetini na bado tutashuhudia mengi sana kwenye ligi ya msimu huu,munhu atupe umri na muda ili tuje kua mashuhuda.
ReplyDeleteMdogo wake nani?Mtibwa timu nzuri sio wa kuilinganisha na timu ya mwisho kwenye ligi.KMC waliwapiga 4G kama wamesimama.Eti Amri Saidi.Hamkosi visingizio vya refa.Litimu libovu. Afadhali hata ya msimu uliopita. Anzeni kutafuta mchawi na visingizio.
ReplyDeleteKama bovu lako?lkn jua utabakwa tu hata Kama hutaki.
ReplyDeleteTimu bovu lkn kila mcheZaji wa Mbeya City akihisi kachezewa faulo analala akingoja kutibiwa kwa mchezo ule ikitokea mara nane sasa Hiyo ninyi wachunguliaji Ina maanisha mlikuwa mnaangalia mpira akina mama wameshika nyonyo na Wanaumme Korodani mkiombea sare na mkifurahia walivyo kuwa wanapoteza mudA.Na kuthibitisha kuwa walikuja na mbinu hovu yule captain wAo alihojiwa baada ya mchezo anasema yeye Kama mchezaji hajui mipango ya mchezo hujao anayejua ni Mwalimu.Hii inatafsiriwa kuwa mood ya Mwl inategemea Ni mchezo gani na Timu hipi.Na Mwl alisema tulikiwa dhaifu Kwenye ulinzi na katikati siku ya KMC nimebanwa mabadiliko sita kuondoa udhaifu uliyo jitokeza.Lkn pamoja na ubora walionyesha na kutumia nguvu nyingi tabia ya kujiangusha ilikuwa moja ya mbinu yao na baada ya kufungwa hawakulala Tena Mikia mpooo
ReplyDelete😆😆😆 kupoteza muda nimojawapo ya mbinu ya michezo ya ugenini. Utopolo mpo tutawaangali kaitaba nako mtachezaje
Delete