September 13, 2020

 


JANA mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba walibanwa mbavu kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Uongozi wa Simba umesema kuwa matokeo hayo yanaweza kuonekana sio mazuri kwa kuwa ni sare ila kutokana na mazingira ya miundombinu hamna namna ya kufanya.


Simba ilianza kufunga bao jana, Septemba 12 kupitia kwa kiungo mzawa, Mzamiru Yassin dakika ya 44 na liliwekwa sawa na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar dakika ya 46 Boban Ziringatus .

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:"Yaweza kuonekana matokeo sio mazuri kwa kuwa tumepata  sare. Kupata pointi nne away(ugenini) katika viwanja kama vile ni kitu cha kushukuru pia."


Mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 2-1 mbele ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine na mchezo wa pili imekwama kusepa na pointi tatu kama ilivyotokea kwa wapinzani wao Mtibwa Sugar kukwama, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

16 COMMENTS:

  1. Mazingira yana ugeni gani kwa timu zetu, miaka nenda rudi viwanja ndo hivi na ubingwa mnachukua huko, Leo ghafla mazngra duh!

    ReplyDelete
    Replies
    1. .......Na msimu uliopita tuliifunga Mtibwa 3-0 uwanja huo huo wa Jamhuri!

      Delete
    2. Makocha wajitathmini mbinu za mazowea si njia sahihi kwa soka la kisasa. Kama mfumo hautoi matokeo ubadilishwe. Makocha na wachezaji wa timu pinzani wameshaisoma Simba kwa hiyo Sven na Matola waangalie kubadili mbinu na kutumia wachezaji wote kwa kutazama nani anaweza nini

      Delete
    3. Hivi simba imeshinda mechi moja ime droo mechi moja hivi hiyo misimu yote tunayochukua ubingwa simba huwa anashinda mechi zote, hii nchi ni ngumu sijawahi kuona na kama mashabiki wa hizi timu hawatabadili fikra zao kuhusu mchezo wa soka basi tuna kazi ngumu sana kufika tunapopataka hakuna ligi duniani timu inashinda tu leo hii tumecheza mechi mbili eti kwa sababu ya maneno ya manyani fc na washabiki wa simba wanaingia kwenye mkumbo huo huo wa kulaumu benchi la ufundi, mkiwasikiliza mashabiki wa Manyani fc mnafeli wao wameshashindwa kucheza mpira uwanjani kilichobaki sasa wanataka kushindana na nyinyi maneno, na hamuwezi kuwashinda kwa maneno kwa sababu wengi ni waimba taarabu, mara simba inapulizia madawa, mara simba wananunua mechi, mara TFF simba yani hawana hoja ya msingi

      Delete
  2. Manara kikosi mnashindwa kukitumia vizur. Kunacombination hazijakaa sawa. Badilisheni mfumo sio viwanja

    ReplyDelete
  3. Huo uwanja mwaka jana tulishinda 3-0 acheni visingizio Kocha alishindwa kupanga kikosi,Chama mpira ulimkataa bado kishingo hakumtoa.

    ReplyDelete
  4. Viwanja ni tatizo na aibu kwa nchi na mpira wetu.

    ReplyDelete
  5. Mtibwa wa mwaka jana sio wa mwaka huu hilo mlitambue

    ReplyDelete
  6. Hakuna timu isiyopoteza duniani, ni dharau kubwa kuona timu kama Mtibwa haiwezi kuwepo na Simba. Usajili mzuri usitupe kiburi na majivuno
    Kama tunajiona tunaweza shinda mechi zote basi tuwaambie TFF wafute ligi watupe kombe sababu hatuna timu ya kucheza nayo Tz

    ReplyDelete
  7. Viwanja ndio hivyo hadi ubingwa mara 3 leo viwanja vibovu mfungaji bora mara 2 mfululizo anawekwa benchi sijawahi ona ujinga kama huu safari hii tukiwa wa 3 bahati kabisa na huko club bingwa raundi ya kwanza tu tunatolewa tena kwa aibu kubwa tupo mtakuja kukumbuka haya maneno yangu mm ni mwanachama

    ReplyDelete
  8. Wewe sio mwanachama na mpira hujui na hutakuja kujua mpira ukiwa mshabiki wa mihemko, kwa hiyo leo hii unataka simba ashinde mechi zote basi hakuna maana ya kuwa na ligi, ametoa droo tena na timu ambayo imeshawahi kuwa bingwa mara mbili kwenye kiwanja amabacho hakiruhusu simba kucheza mpira wake iliouzoea, eti safari hii tukiwa wa 3 bahati yani hii nchi imejaa mazuzu sijawahi kuona.

    ReplyDelete
  9. Huu ushabiki mwingine WA ajabu Sana huwezi kusingizia viwanja kwa hao mliocheza nao walitumia uwanja upi?mechi ya mtibwa enzi za uchebe tulishinda 3-0 Na mwaka Jana Na kishingo 3-0,Leo hii uwanja?.Tumecheza Na namungo uwanja WA kigoma mbovu tukashunda,Juzi ngao ya jamii Arusha tumeshinda,uwanja WA karume Ni mbovu Sana kuliko WA jamuhuri nipo Arusha naujua vizuri,Kocha alishindwa kupanga kikosi kizuri Chama haikuwa siku yake mpira ulimkataa hadi aibu nikajiuliza wapi Dilunga aliyekulia manungu?aliyeuzoea uwanja Na kusaidia kuifumua mtibwa 3-0 enzi za Uchebe?

    ReplyDelete
  10. Wiki 2 zilizopita Manara aliwaambia Yanga, akiwashauri wajiandae kulalamika; kwamba wakati Simba wameanza mazoezi, wao (Yanga)wanazurura. Kwamba ligi ikianza Simba itashinda mechi 28 mfululizo kwa "clean sheet"; niliizingatia sana kauli hii kwa kumzoea Kocha wa Yanga aliyepita kulalamikia viwanja, waamuzi na TFF.
    Sasa kwa michezo ya raundi ya pili tu Manula kafungwa kila mechi na pia kuna asante refa ya bao la 2 la Ihefu. Wakati nikiichukulia hii kama hsla ya kawaida ya mchezo Manara kaibuka na issue ya viwanja!
    Mmmh asije Haji akaanza kuingia kwenye channel zilezile!

    ReplyDelete
  11. Mimi mwenye hii blog kariri namba yangu nimekwambia mnatumiwa na mna mtumia Haji vibaya.Huyo jamaa kajiripua Sana kila analosema mkaona anajua Sana mtaaibisha Fani zenu,wapenzi wengi wa Simba wamekuwa wehu cse wanamsikiliza Sana.Hapa leo kichwa Cha habari Uongozi wa Simba watoa sababu za matokeo ndani una mnukuu Msemaji wa Timu,niliuliza Jana je Uongozi au Bodi ya Simba ndiyo ilimwagiza atoe sababu za Yanga kutopata matokeo,na je Ni halali yeye kama msemaji wa Simba kuita media akaongelea udhaifu wa Yanga kwa mchezo hule? Zingatia haikuwa mechi kati ya Yanga na Simba na akahukumu akaita wazururaji na ninyi na Uandishi wenu wa ki Friend of Simba mnajisahau kwa hilo.Ukweli ni kwamba tutasoma hizi blog cse hatuna jinsi lkn hii tathnia ya habari za michezo mnakwaza Tena sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic