December 17, 2020

 




UONGOZI wa KMC umesema kuwa maamuzi ya penalti iliyotolewa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jana, Desemba 16 hayapo mikononi mwao kwa kuwa hiyo sio kazi yao.

Wakati ikiyeyusha pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba, bao hilo lilipatikana kwa mkwaju wa penalti dakika ya 73 baada ya mwamuzi wa kati Elly Sassi kutafsiri kwamba mchezaji wa KMC aliunawa mpira huo.

Bao la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 77 na na kuifanya timu hiyo kufikisha jumla ya poiinti 35 ikiwa nafasi ya pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Habib Kondo, Kocha Msaidizi wa KMC amesema:" Kuhusu maamuzi ndani ya uwanja hilo benchi la ufundi hatujui, sisi kazi yetu ni kufundisha timu ili ipate matokeo na ndicho ambacho tunakifanya wakati wote.


"Ninachokijua mimi ni kwamba wachezaji wetu walipambana katika kusaka matokeo na tumepoteza hakuna cha kubadilisha zaidi ya mipango kwenye mechi zetu zijazo,".

Tukio hilo  lilichukua dakika nne kwa wachezaji wa KMC kuwa kwenye ubishani na mwamuzi kwa kuwa hawakukubaliana na kitendo hicho .

26 COMMENTS:

  1. Hii tabia ya waamuzi wetu kuharibu mchezo wa mpira kwa ajili ya mahaba sijui wataacha lindi

    ReplyDelete
    Replies
    1. ILE NI PENATI HALALI HATA KAMA INGEWEKWA VAR

      Delete
  2. Penati mbili alizikataa za wazi mungu kamlaani mulemule

    ReplyDelete
  3. Ilichofanya Simba SC ni kuibaka KMC wazi wazi. AIBUUUUU

    ReplyDelete
  4. Msiojua mpira mnalalamika sana kwamba mbeleko hivi una habari kmc walidhamilia kuwavunja wachezaji wa Simba hivyo mwamuzi angefata Sheria kadi nyekundu zingewahusu hata mbili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari za kadi hazi2husu kikubwa n mbeleko fc

      Delete
    2. MAPENZI YASIKUZIDI HISIA, KUSHINDA SIMBA MBELEKO AKISHINDA YANGA MNASEMA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO, WAPUMBAVU NYIE

      Delete
    3. Unayesema KMC walidhamiria kuwavunja miguu wachezaji wa Simba inabidi ukapimwe mkojo! Hiyo dhamira walikushirikisha wewe?

      Delete
    4. Kwani refa alikushirikisha kuwa anaibeba simba, kama ulivyoona penalty na mwenzio kaona rafu za kipuuzi zilivyokuwa zinafanywa. Chukueni hiyo penalty mnayolilia mtuachie goli letu la Mugalu

      Delete
  5. Nguruwe fc sasa mmezidi jamani, jana kiukwel mlizidiwa ujanja basi nae Refaree baada ya kuona ndo hivyo tena basi akaamua kuwabeba ila kila mtu aliona kuwa haikuwa penaliti halali, siku zote machozi ya binadaamu mwenzio ni laana kubwa sana, ili kudhihirisha haya mtapigwa na FC PLATINUM, NAMUNGO na mnatoa droo na AZAM

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wambieni TFF watunge sheria penalt wawe wanapewa Utopolo tu labda mtaridhika wataalam wa kulalama

      Delete
    2. Pelekeni malalamiko yenu fifa, mnapumuliwa mgongoni sasa mnaanza kuweweseka mwenye nafac yake anakuja jiandaeni kunyanyuka hpo siyo penu. Kimataifa subirini tuwabebe Hamna uwezo wakujibeba wenyewe nyie viazi uto.

      Delete
    3. Sasa mtu analilia penalty wakati hakumbuki ndani ya box aliingia lini mara ya mwisho. Kama ni makosa walianza Kmc kuwaruhusu simba waingie kwenye 18

      Delete
  6. Wewe Utopolo penalti ya Simba inaweza hata kujadilika.Mliopewa mkicheza na KMC Kirumba Mwanza haikuwa hata kwenye box.Ila sisi Simba huwa hatuangaiki na matokeo yenu. Kila Simba akicheza mpo roho mkononi. Mpaka mmeweka rekodi ya ujinga ya kuwapokea Plateau.Hivi mliwasindikiza?
    KMC wenyewe wanasema uamuzi wa refa wao hawazungumzii. Nyie punda wa mbele mnapiga yowe aliyepigwa mjeledi ni punda wa nyuma.
    Maajabu.

    ReplyDelete
  7. Kaseja aliyekuwa karibu kasema hakushika, lakini refa akaona awabebe...mbeleko s.c.

    ReplyDelete
  8. wewe habibu kondo ni mnafiki sana, mm nilikuwa nakusubiri kwa hamu utasema nn juu ya ile penalty feki. Siku ya yanga uliongea porojo kibao kuhusu ile penalty feki ya yanaga, leo umewaachia waamuzi. Sasa kwann na ile ya yanga hukuwaachia waamuzi uliongea porojo zako? Acha usimba wako umeshazea kidude kalale. Hii Tanzania ni simba na yanga tu nyinyi wengine ni moto wa kifuu tu

    ReplyDelete
  9. Kama ni hivyo basi tuseme kmc wanabalaa maana mechi waliocheza na yanga yanga walipewa penait na hii ya simba munasema pia simba kapewa penait.musiangalie upande mmoja.

    ReplyDelete
  10. Hakuna anayewajua wanafamilia vizuri kama mwanafamilia.Eymael aliwaita Yanga mbumbumbu na akawaita wanyama fulani fulani..hakika hakukosea hata kidogo...Alipatia saanaa..
    Sasa hivi sheria ni mpira ukigusa mkono..haijalishi nini kilifuata kingine.
    Inakuwaje penalti ikitolewz kwa Yanga sio tatizo..ila Simba ikipata ni taabu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Morisson kawanyooshea kidole huko hamumpangi mikia mulimtoa kwa mmbwembwe sasa munampotezea

      Delete
    2. Simba sio Yanga kwamba kila mechi mchezaji atacheza..Morrison kacheza Nigeria na Dar na hata Mbeya alicheza...hujui unachoongea..Kahata,Bwalya, Kagere na wengine wengi hukaa benchi.Yanga wajaribu basi kupumzisha wachezaji wao uone kama hata hilo goli moja watalipata..Vipi mlishapata mil 600 za Morrison?

      Delete
  11. Malalamiko fifa, humu mnatupigia kelele tu.

    ReplyDelete
  12. Kazi ya referee hiyo,yeye ndo mtafxiri wa xheria 17 za xoka, wengine waxhangiliaji tu .ximba oyeee! !

    ReplyDelete
  13. Kuna mtu anateseka.... Utopolo mnakwama wapi nyinyi

    ReplyDelete
  14. 𝐇𝐞𝐫 𝐬𝐚𝐬𝐢𝐢 𝐧 𝐦𝐢𝐨𝐧𝐠𝐨𝐧 𝐦𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐚𝐦𝐮𝐳 𝐰𝐚𝐳𝐮𝐫 𝐭𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐢𝐥𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐜𝐡𝐞𝐳𝐨 𝐰𝐚 𝐣𝐚𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐥𝐢𝐤𝐮𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐬𝐡𝐢𝐦𝐨 𝐦𝐞𝐧𝐠𝐢 𝐬𝐚𝐧𝐚

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic