July 29, 2015


Mzee Moshi Shabani amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.


Moshi ndiye baba wa wanasoka maarufu nchini ambao ni Mrisho Moshir, Iddi Moshi ‘Mnyamwezi’, Ally Moshi na Haruna Moshi ‘Boban’.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Mnyamwezi alisema mzee wake amefariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.

"Mzee katutoka, Mwenyezi Mungu amemuhitaji leo saa sita na nusu mchana. Tunatarajia mazishi yatakuwa kesho mchana, inshallah" alisema.

Marehemu ambaye alikuwa mwajiriwa wa muda mrefu wa Shirika la Reli Tanzania, amefariki baada ya kuugua muda mrefu.


Taratibu za mazishi zinaendelea na tutawataarifu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic