Timu ya taifa
ya Tanzania ya Wanawake cwenye umri chini ya miaka 20 'Tanzanite' kesho siku ya
jumamosi itashuka dimbani uwanja wa Azam Complex kucheza na timu ya Taifa ya
Zambia chini ya miaka 20 (Young She-Polopolo).
Viingilio vya
mchezo wa kesho kati ya Tanzanite dhidi ya Young She-Polopolo ni shilingi elfu
mbili (2,000/=) kwa jukwaa la mzunguko, na shilingi elfu tatu (3,000/=)
kwa Jukwaa Kuu.
Mchezo huo wa
kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Kombe la Dunia zitakazofanyika
mwakani nchini Papua New Guinea, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini
Sudan,unatarajiwa kuanza saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na
kati.
Timu ya Young
She-Polopolo tayari imeshwasili nchini jana jioni, na leo wakitarajiwa kufanya
mazoezi mepesi leo jioni katika uwanja wa Azam Complex kw ajaili ya mchezo huo.
Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Sudan tayari wameshawasili.
Wakati huo
huo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetoa usafiri wa mabus mawili
kwa ajili ya kikundi cha ushangiliaji cha timu za Taifa (Taifa Supporters)
kitachokwenda kesho Chamazi kuipa sapoti timu ya Tanzanite.
Mabasi hayo
mawili yataondoka ofisi za TFF zilizopo Karume saa 6 kamili mchana kuelekea
Chamazi kwa ajili ya kuishangilia timu ya Taifa ya wanawake chini ya
miaka 20 (Tanzanite).
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
0 COMMENTS:
Post a Comment