Beki kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameibuka na kusema
kuwa beki a pembeni wa timu hiyo, Joseph Zuttah, anahitaji kupewa muda ili
aweze kuenda sawa na timu hiyo.
Zuttah, raia wa Ghana, alionyesha kiwango kidogo katika michuano
ya Kombe la Kagame kiasi cha kuwafanya mashabiki wamchukie na kumjadili kila
kona.
Cannavaro ambaye ni nahodha wa Yanga, amesema kuwa ni vigumu kwa
upande wake kumjaji mchezaji kwa muda mfupi na kudai kuwa anachoamini yeye,
mchezaji huyo ni mzuri lakini anahitaji muda ili aweze kufiti na wenzake.
“Kwa upande wangu, Zuttah namuona ni mchezaji mzuri na mwenye
uwezo, lakini ni vigumu kuweza kumjaji mtu kwa mechi chache tu alizocheza.
‘Bado anahitaji muda wa kuweza kuwa vizuri baada ya kuzoeana na
wenzake, lakini kwa upande wangu, namuona ni mchezaji mzuri na hana shida
yoyote,” alisema Cannavaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment