LENGO kubwa la usajili wowote ule ni kuboresha pale ambapo palionekana kuna mapengo kwenye timu fulani kwa kuongeza mchezaji.
Siku 30 za usajili wa dirisha dogo la usajili Bara zilifungwa wiki iliyopita huku ikishuhudia timu karibu zote zikiwa na maingizo ya wachezaji wapya vikosini mwao. Lakini katika usajili huo kuna sajili ambazo zinaonekana kuwa bora zaidi kama ifuatavyo;
Kipa: Mathias Kigonya –
Azam
Licha ya kuwa na orodha pana kidogo ya makipa ambao
wamesajiliwa kwenye dirisha hili lakini Mganda Mathias Kigonya ndio unaonekana
kuwa bora zaidi.
Kipa aliyetua Azam FC akitokea Forest Rangers ya Zambia licha
ya kudaka lakini pia anafunga, akiwa amekuja kwa ajili ya kuwasaidia David
Kissu na Benedict Haule.
Makipa wengine waliosajiliwa dirisha hili ni Deogratius
Munishi (Ihefu), Ally Mustapha (Mbeya City) na Peter Manyika (Dodoma Jiji).
Mabeki wa pembeni;
Edward Manyama na Ally Ally
Usajili wa Edward Charles Manyama kutoka Namungo kwenda Ruvu
Shooting umewashtua wengi, kwani haukutarajiwa kutokea lakini haumuondoi beki
huyo kuwa kwenye kikosi hiki anaingia kama mlinzi wa kushoto.
Lakini pia Ally Ally ambaye ametua Coastal Union akitokea
kwao Zanzibar unamfanya awe miongoni mwa wachezaji ambao wakiunda kikosi cha
usajili bora basi atakuwepo akiwa kama mlinzi wa kulia.
Mabeki wa kati; Job na
Kelvin Yondani
Hapa hakuna shaka yoyote kwamba mabeki hawa wanastahili
kuanza katika kikosi hiki wakiwa kama walinzi wa kati. Yondani amerejea kwenye
ligi akisaini Polisi Tanzania baada ya kutokuwa na timu kwa miezi sita.
Job ametua Yanga akitokea Mtibwa Sugar ambapo amesaini
mkataba wa miaka miwili na nusu.
Kiungo mkabaji; Taddeo
Lwanga
Kiungo huyu raia wa Uganda kasi yake inaonekana kuongezeka
kila baada ya mechi tofauti na mwanzoni wakati anaanza kucheza.
Lwanga amesaini Simba na kumwaga winbo kwake ndani ya
Msimbazi kunamuweka katika kikosi cha usajili bora ambao umefanywa kipindi cha
dirisha dogo.
Kiungo mchezeshaji;
Raphael Daud
Kiungo huyu amerejea tena uwanjani akiwa na Ihefu SC baada ya
kutokuwa na timu tangu kuanza kwa msimu huu. Licha ya kwamba hajacheza lakini
kama pakiundwa kikosi cha usajili bora basi Raphael hawezi kukosa nafasi kwenye
eneo la kiungo mshambuliaji.
Mawinga; Perfect
Chikwende na Erick Kwizera
Hawa wote ni wageni, mmoja akitokea Zimbabwe na mwingine
Burundi. Wote wameonyesha pafomansi nzuri ambapo mabosi wa Simba walipagawa
Chikwende akiwa FC Platinum ambapo aliwafunga na mwisho wakamsajili.
Kwizera raia wa Burundi alithibitisha uwezo wake kwenye Kombe
la Mapinduzi akiwa na jezi za Namungo kiasi mabosi wa klabu hiyo wakampa
mkataba. Katika kikosi hiki wawili hawa ndio watakuwa mawinga.
Washambuliaji; Reliants
Lusajo na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’
Mabwana hawa ndio ambao watasimama eneo la ushambuliaji na
tayari kila mmoja kazi yao wameshaionesha. Lusajo akiwa na KMC kabla ya kutua
Namungo alifunga mabao manne.
Saido ameshafunga mabao mawili na ana pasi tatu za mabao hadi
sasa ikiwa ni baada ya kusajiliwa Yanga akiwa mchezaji huru.
Wachezaji wa akiba
Deogratius Munishi ‘Dida’ (Ihefu), Yusuf Mlipili (Kagera
Sugar), Yahya Zayd (Azam), Fiston Abdoul Razak (Yanga), David Mwasa (Mbeya
City) na Mrisho Ngassa (Gwambina).
Mmeishiwa vya kuandika sasa mkurupuka tu
ReplyDeleteMvuta bangi mbichi huyu. Hana cha kuandika kabisa.
ReplyDeletekweli huyu alieandika hayo mavi ni mvuta bangi tena ile ya Arusha, hii brog kwakwel na wasiwasi na taaluma za wandishi dah upuuzi gani huu
ReplyDeletemavi tu et kikosi
ReplyDeleteWamekosea wap achen kutukana hovyo
ReplyDeleteHata Mimi sijaridhishwa na prediction zao
ReplyDeleteUgolo tu mkalale
ReplyDeletenaona vtu vya kuandika mmeishiwa
ReplyDelete