Beki
wa kulia wa Simba, Ramadhani Kessy amsema kikosi chao kiko safi kuliko watu
wanavyoamini.
“Simba
iko katika kiwango kizuri na tunaendelea kujifua, mimi ninaamini kama kila kitu
kitaenda katika mpangilio mzuri basi tutatoa upinzani mkubwa tu.
“Watu
wasitudharau wakiamini kwamba hatuna kitu au hatuwezi kufanya vizuri,” alisema.
Simba
imeonyesha kiwango kizuri na kufanya vema katika mchi zake zote za kirafiki
mjini Zanzibar.
Kessy
amekuwa kati ya wachezaji wenye kiwango kizuri na mwanzo wa mashambulizi katika
kikosi hicho kutokea upande wa kulia.
Simba imeweka kambi mjini Zanzibar ikiwa ni maandalizi yake ya mwisho kujiandaa na Ligi Kuu Bara, itarejea Dar es Salaam wikiendi hii kwa ajili ya Simba Day.
0 COMMENTS:
Post a Comment