January 20, 2016



Mshambuliaji Mganda, Hamisi Kiiza ameonyesha kweli ni mtambo wa mabao baada ya kufunga bao la 10 na kumfikia mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga.

Kiiza raia wa Uganda amefunga bao moja wakati akiiwezesha kuitwanga JKT Ruvu kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.

Bao la pili la Simba lilifungwa na Dani Lyanga lakini Kiiza akaanza kwa kufunga bao lake la kumi kwa mkwaju wa penalti na kumfikia Kiiza raia wa Burundi aliyekuwa anaongoza kwa mabao 10.

Mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar, Kiiza alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 na kumvuka  Donald Ngoma raia wa Zimbabwe mwenye mabao nane lakini akawa amemfikia Elias Maguri mwenye mabao tisa na leo amefunga tena moja na kumfikia Tambwe.


Kiiza ndiye alianza kwa kasi juhudi za ufungaji, baadaye akaanza kusumbuliwa na majeraha, hali iliyompa Tambwe nafasi ya kumpita kwa idadi ya mabao kabla ya yeye kufunga mabao mawili katika mechi mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic