September 3, 2020


MEDDIE Kagere, mshambuliaji namba moja wa Klabu ya Simba amesema amesikitishwa na taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa amempiga kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck.

 

Septemba Mosi taarifa za Kagere kudaiwa kumpiga kocha huyo kisa kikiwa ni kutopangwa kikosi cha kwanza cha Simba zilizagaa kwa kasi mitandaoni, na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

 

 Mshambuliaji huyo amesema ameshangaa baada ya kuona mambo hayo yanasambaa wakati yeye hajafanya tukio hilo.

 

“Kuna mambo huwa yanasemwa kuhusu mimi ambayo siyo ya kweli yenye lengo la kunichafua ndiyo maana sijawahi kuwajibu.


“Lilianza la hirizi nikanyamaza na sasa limekuja la mimi kupigana na kocha kitu ambacho siyo kweli. nashangaa sijui mwalimu nimempiga wapi,” amesema Kegere.


Uongozi wa Simba SC kupitia Ofisa Habari Haji Manara umekanusha taarifa hizo kwa kusema hazina ukweli, zaidi ya kutaka kuvuruga amani ndani ya kikosi chao ambacho kipo tayari kuanza kutetea taji la Tanzania Bara mwishoni mwa juma hili dhidi ya Ihefu FC.

 

Haji Manara amesema: ”Wanasema ugomvi uliotokea mazoezini, lakini Simba hawakuwa na mazoezi baada ya mchezo wa ngao ya jamii, hizo ni propaganda za kuvuruga utulivu uliopo ndani na nje ya Simba, wakitaka itokee kama upande wa pili yanayoendelea.

 

“Kama idara ya Habari na Mawasiliano hatutokubali kuona watu wanaandika uzushi kuhusu klabu yetu na tutachukua hatua kali dhidi ya watakaohusika.”

13 COMMENTS:

  1. Hawajapata walichokusudia hawa wazushi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona mnaficha ukweli kama kamdunda kocha ni Sawa tu

      Delete
  2. Haji ana moyo aisee! Yani anatumia nguvu nyiiingi kwa tetesi tu je likiwa jambo la kweli si atakufa na presha?

    ReplyDelete
  3. Ni dhahiri Yanga wanawahofu sana hawa watu wawili ndani yw simba yaani kagere na Sven si ajabu kuona yanga wanawatenezea majungu. Sven ni kocha na simba wangejipindua tu Kwa Sven na kumuacha aondoke basi hivi sasa ni kocha wa Yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe huna akili yaani yanga wamuhofie kagere a.k.a babu Yule?

      Delete
    2. Kila kitu yanga mnamsingizia kupigana mpigane wenyewe halafu mnasema yanga

      Delete
  4. Yanga wanahaha, misimu miwili mtungaji Bora unafikiri mchezo, sasa na mwaka Garrick hiyooo ababeba Tena. Sven Ni noma kocha kijana anayejitambua utopolo mnaishia kufukuza makocha na huyo naye baada ya tarehe 18/10 out

    ReplyDelete
  5. Kagere ndo kwanza ongeza cheche kudadeki piga 30 magoli mwaka huu utopolo wakanywe sumu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Babu kagere anataka kuamkiwa na kocha wake ndio sababu ya kumpiga kishingo

      Delete
  6. Huna cha kuandika tangia juzi ni kutengeneza stori za kagere tu kama huna cha kuandika acha waandike hao wanao kutuma

    ReplyDelete
  7. Ukweli ni upi?, piga sana kelele ili iwe kweli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic