February 28, 2013




Askari Polisi wa Catalan wanakotokea Barcelona, wametoa mpya ya mwaka baada ya kufanya jitihada kubwa ili kupata jezi na bukta chafu za wachezaji wa Real Madrid.

Askari Polisi hao maarufu kama Mossos d'Esquadra, walibaki kwenye milango kwenye uwanja wa ndege wakati Real Madrid wakiondoka mjini hapo kurejea kwao baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Kwa kuwa askari hao ndiyo walipewa kazi ya kuhakikisha Madrid wanakuwa salama hadi watakapoondoka kwenye uwanja huo wa ndege, waliitumia nafasi hiyo kuomba vifaa hivyo ambavyo walivitumia katika mechi hiyo.

Pamoja na kujulikana wengi wao ni mashabiki wa Barcelona, lakini walitumia muda wao mwingi kumpongeza Jose Mourinho na wachezaji wake kwa ushindi huo mkubwa ambao umeonekana kama aibu kwa Barcelona.

Wachezaji wengi wa Madrid walikuwa wakiendelea na sherehe, tokea siku iliyopita ambayo walishinda mechi hiyo hadi kesho yake wakiwa wanaondoka kurejea Madrid.

Tayari Madrid imeanza kujiandaa na mechi inayofuata dhidi ya Barcelona ambayo lazima watatakiwa kushinda bila ya kujali ugenini ili kufuta aibu iliyowakuta katika mechi ya Kombe la Mfalme ambayo sasa wametolewa na Madrid wametinga fainali na tayari wanajua watawavaa wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid katika fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic