February 28, 2013




Baada ya mashabiki kuendelea kumsakama mfululizo, Kocha Mkuu wa Chelsea, Rafa Benitez ameamua kuwatolea uvivu mashabiki wa Chelsea na ‘kuwaangushia’ mbofumbofu.

Benitez amewaambia mashabiki wa Chelsea ni watu wa ajabu ambao wanaishambulia timu yao bila ya kujali lolotea.

Amesema anashangazwa na mashabiki hao ambao wamekuwa wanamshambulia tokea alipochukua timu Novemba mwaka jana bila ya kujali maendeleo ya timu.

“Sijawahi kuona mashabiki wa namna hii, badala ya kujiandaa kuja kushangilia timu wanapoteza muda kutengeneza mabango ya kunishambulia na kuisakama timu.

“Niko katika soka kwa miaka 26 sasa, nimebeba ligi ya mabingwa, Kombe la FA, Italia Super Cup na Ubingwa wa Hispania mara mbili. Vipi leo naonekana kama kocha ninayeanza kazi.

“Wanasababisha presha kubwa kwa mashabiki, hawawezi kutulia tena. Wakiendelea hivi, mwisho mwakani timu itacheza Kombe la Europa kwa kuwa wachezaji wanakuwa hawajiamini,” alisema Benitez.

Mashabiki wamekuwa wakimsakama Benitez tokea achukue timu hiyo wakionyesha kutokubaliana na kuondolewa na Di Matteo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic